Mwenyekiti Kamati ya ulinzi na usalama Tarafa ya Mihambwe ambaye pia ni Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu mapema leo Februari 22, 2022 amewafariji wakazi wa vijiji vya Mihambwe na Ruvuma kufuatia jana Jumatatu Februari 21, 2022 kutokea kadhia ya upepo mkali uliombatana na mvua kubwa ulioezuea paa za nyumba 15, Madarasa 8, ofisi 3 na nyumba 2 za Waalimu. Shule zilizopatwa na kadhia hiyo ni shule ya msingi Mihambwe na shule ya msingi Ruvuma ambazo zipo vijiji vya Mihambwe na Ruvuma.

"Kwanza nawapa pole kwa Wananchi, Waalimu na Wanafunzi wote waliopatwa na majanga ambayo yalijeruhi Mtu mmoja na hakuna kifo.

Nikiwa kiongozi wenu wa Tarafa nimeguswa na kuamua kufanya ziara hii fupi kujionea hali halisi, kuwapa pole na kuwafariji. Serikali ipo pamoja nanyi bega kwa bega kuhakikisha Watoto wetu wanaendelea kusoma kama awali, miundombinu ya Madarasa inarejeshwa vyema haraka iwezekanavyo kama ilivyokuwa awali na Wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida". Alisema Gavana Shilatu

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na uongozi wa vijiji na shule kutembelea makazi na Madarasa yaliyopata uharibifu mkubwa ambapo aliongea na Viongozi, Wananchi, Waalimu na Wanafunzi ambao wameonyesha utulivu mkubwa na ushirikiano nyakati zote.

Share To:

Post A Comment: