Takribani wananchi wanaopindukia 139 katika mtaa wa Mjimwema halmashauri ya mji wa Njombe waliolipia huduma ya kuunganishiwa nishati ya umeme wamefanikiwa kupata nishati hiyo kupitia kampeni ya ''tumejipanga,kutana na TANESCO nyumbani kwako'' inayotekelezwa mkoani humo kuhakikisha wateja wanapata umeme katika kipindi cha mwezi mmoja.

Baadhi ya wananchi walioingiziwa nishati ya umeme akiwemo Hamidu Hamis,Aisha Mohamed na Abas Sanga waliounganishiwa umeme wamesema hatua ya TANESCO kupelekea nishati ya umeme kumewarahisishia upatikanaji wa wateja wa nyumba za kupanga pamoja na kuwapunguzia adha waliyokuwa wakiipata pindi wanapotumia umeme wa solar.

“Jana nimepigiwa simu kutoka TANESCO kwamba wanakuja kunifungia umeme na kweli huduma hii imekmilika leo,niwashukuru sana kwa huduma nzuri nay a haraka zaidi kwasababu awali hapa nilikuwa natumia sola”alisema Hamidu Hamis

Abas Sanga amesema “Kwanza hizi nyuma nimezijenga nilipostaafu kwaajili ya kupangisha na nyumba amabyo haina umeme watu hawapendi kupanga ninashukuru sana TANESCO kwa huduma yao ya kuniunganishia umeme leo

Meneja wa shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Njombe mhandisi Jahulula Maendeleo anasema zoezi hilo litakwenda katika wilaya zote za mkoa wa Njombe kuhakikisha wananchi wote waliolipia fedha yao wanafikiwa na huduma ya umeme.

“Wananchi ambao walilipia na kusubiri huduma sasa watapata fursa ya kufungiwa umeme”alisema Mhandisi Jahulula Maendeleo

Neema Didas Lyakulwa ni afisa uhusiano TANESCO mkoa wa Njombe amewaelekeza wateja wao jinsi ya kutumia nishati hiyo.

Februari 23 mwaka huu zoezi hilo linafanyika katika kijiji cha Itunduma na kuelekea Maguvani mjini Makambako pamoja na maeneo ya Mtwango ndani ya wiki hii.

Mafundi wa umeme kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wakifunga umeme kwenye moja ya nyumba ya mteja iliyopo mji mwema mjini Njombe

 

Share To:

Post A Comment: