OR-TAMISEMI


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua  uteuzi wa Wakurugenzi 4 wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya Fedha za miradi ya maendeleo hususan ni zile za Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.


Wakurugenzi hao ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza, Manispaa ya Singida - Mkoani Singida, Halmashauri ya Jiji la Mbeya - Mkoani Mbeya na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.


Akizungumza mbele ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zimetuhuniwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi uchunguzi umefanyika na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita uchunguzi unaendelea.


Mhe. Rais  Samia ameagiza uchunguzi uendelee katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo napo kuna tuhuma za namna hiyo.

Share To:

Post A Comment: