Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dar es salam wakati akizindua kipindi maalum cha ”Kilimo kwanza” kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha Televisheni cha TVE kwa lengo la kuhamasisha kilimo miongoni mwa vijana na kutoa taarifa muhimu za kilimo.

Nawapongeza sana TVE kwa wazo hili la kuamua kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza kilimo nchini.

Kipindi hichi kitasaidia sana kuhamasisha matumizi ya sayansi na kanuni bora za kilimo ili wakulima wetu walime kwa tija.

Pia kipindi hichi cha Kilimo Kwanza cha TVE kitakuwa kinaongeza taarifa na maudhui zaidi ya kilimo ambayo tutayarusha kupitia TBC kwenye chaneli ya Kilimo ambayo tunatazamia kuianzisha hivi karibuni itakayojikita kutoa elimu kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kanuni bora za kulima na matumizi sahihi ya pembejeo kwa wakulima” Alisema Mavunde.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Afisa Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa EFM & TVE Ndg. Francis Sizza “Majizzo” amesema lengo kubwa la kipindi hiki cha kilimo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza kilimo na kwamba wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahamasisha vijana wa vijijini na mijini kushiriki katika kilimo ikiwemo wasanii wakubwa wa muziki na filamu nchini kama sehemu ya kampeni ya kunufaika na mpango wa serikali wa Building a better tomorrow-Toboa na Kilimo .

Share To:

Post A Comment: