Na. Angela Msimbira  NGARA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema  hadi kufikia Januari, 2022 shilingi bilioni 9.3 kwa ajili ya kuendeleza sera ya elimu bila Ada Mkoani Kagera


Ameyasema hayo leo tarehe 22 Februari, 2022 wakati alipohutubia wananchi kwenye maadhimisho ya  Jubilei ya Miaka 25 ya Utumishi wa Kiaskofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Lulenge - Ngara Mkoani Kagera.


Waziri Bashungwa amesema  Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kwa  ajili ya ukamilishaji wa madarasa  ya shule za sekondari  na msingi 167 na  kuwezesha kujenga  maabara 72   lengo ni kupunguza uhaba wa maabara mashuleni. 


 Sambamba na hilo Waziri Bashungwa amesema Mkoa wa Kagera kulikuwa na kata 11 ambazo hazikuwa na shule za Sekondari hivyo, Serikali  imetoa shilingi bilioni 7.7 kwa ajili ya  ujenzi wa shule za sekondari kwenye  kata ambazo hazikuwa na shule za Sekondari.


Waziri Bashungwa ameendelea   kusema kwa Mkoa wa Kagera kiasi cha shilingi bilioni 15 . zimetolewa na Serikali  kwa ajili ya  ujenzi wa madarasa 116 ya shule za sekondari  ambayo yamewezesha  kupunguza msongamano mashuleni.Aidha, amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na taasisi za dini  hasa katika suala la kuleta maendeleo kwa jamii na kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi. 


Amesema kuwa Taasisi za dini  zinashirikiana na Serikali katika maendeleo na kuwahudumia wananchi, hivyo kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI iliunda timu ya kuangalia  maeneo ambayo yanashirikiana na Taasisi za dini katika kutoa huduma mbalimbali  hususani huduma za afya na kuangalia namna ya kushirikiana katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.


Aidha, amechukua nafasi hiyo kumpongea Askofu Niwemugizi kwa kufikisha Jubilei ya Miaka 25 ya uaskofu.

Share To:

Post A Comment: