Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro ametoa wito Kwa viongozi wa Dini kuendelea kuhamasisha waumini na Jamii Kwa ujumla umuhimu wa kuhifadhi na kuyalinda mazingira.
Wito huo ameutoa katika mkutano wa 49 wa kuwajengea mahusiano mema kati ya Dini za Kiyahudi,Kikristo na Kiislamu pamoja na kuangazia Dini na mabadiliko ya tabiachi uliofanyika Wilayani Lushoto.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa Kwa kufanya hivyo ni kutimiza matakwa ya Sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 ambayo imeweka wazi. Misingi ya jumla katika suala Zima la uhifadhi wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa viongozi wa Dini wanaowajibu wa kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kupitia mafundisho ya dini Juu ya kutimiza matakwa ya sera ya mazingira ya mwaka 2021 ili malengo yaliyowekwa na serikali katika sekta ya uhifadhi mazingira yanatimia na Tanzania inakuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya tabiachi.
" Umefika wakati wa kutumia ndimi ,elimu katika kuwaeleza wafuasi kuhusu athari hasi za kimazingira ili kulinda Dunia na viumbe vilivyopo ndani yake.
Alieleza kuwa ardhi ni amana kutoka Kwa Mungu , binadamu ni wasimamizi hivyo Jamii inatakiwa iishi Kwa kuthamini,kulinda na Kutunza mazingira Kwa kujiepusha na uharibifu wa aina yoyote ,ikiwemo uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Aidha alisisitiza kupitia mkutano huo ni lazima washiriki wapate msukumo kutoka kwenye mafundisho Kwa kuzidisha ari ya kuishi katika kijani kibichi, kulinda na kuhifadhi mazingira huku wakiendelea kuimarisha maelewano baina yao na ulimwengu.
Katika kusisitiza utunzaji wa mazingira Alisema kuwa wao kama Wilaya wanatarajia kuanzisha kampeni ya upandaji miti ambapo kila kata itatakiwa kupanda miti laki moja.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la KKT Dk Msafiri Mbulu Alisema kuwa mkutano huo wa 49 umewashirikisha viongozi wa Dini kutoka Tanzania na Zanzibar.
Post A Comment: