Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya mwaka 2022/2023 kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana kushoto ni  Naibu wa Jiji hilo Calvas Joseph
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo
Sehemu ya madiwani wakifuatilia kikao hicho


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

 BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga limepitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Jiji kwa mwaka 2022/2023 ya kiasi cha shillingi za Kitanzania Billion 73 ambazo zitatokana na mapato ya vyanzo vya ndani, ruzuku na wahisani.

Bajeti hiyo imepitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo alisema bajeti hiyo imegusa maeneo yote muhimu kwa maendeleo ya Jiji hilo na wananchi wake 

Alisema kwa upande wa mapato ya vyanzo vya ndani, Halmashauri imekadiria kukusanya kiasi cha shillingi Billion 16, huku nguvu za wananchi katika uchangiaji wa miradi ya maendeleo zikikadiriwa kuwa shillingi Million 824.6, huku fedha za kutoka Serikali kuu na wahisani zikikadiriwa kuwa shillingi Billion 56. 

Akizungumzia mpango wa maendeleo katika mwaka wa  2022/2023 Halmashauri imekasimia kutumia jumla ya shillingi Billion 19.9 kwa ajili ya miradi ya maendeleo  ambapo Billion 13.1 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na wahisani na shillingi Billion 6.7 ni fedha za mapato ya ndani na nguvu za wananchi na michango ya fedha taslim makadirio yakiwa ni million 824.

Alisema kwa upande wa miradi halmashauri hiyo itatumia Billion 6.7 za mapato ya ndani kwa mwaka 2022/2023 katika utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Mfuko wa utoaji mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kiasi cha sh. Billion 1.2, Ujenzi wa barabara za lami kupitia Tarura sh. Billion 1.2, Ukarabati wa kituo cha Afya Pongwe, Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za Msingi na Sekondari, Ukarabati wa masoko ya Makorola, Kisosora na Majengo, Ujenzi wa nyumba za watumishi.

Alisema suala lingine ni Ukamilishaji wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari,

Ujenzi soko la samaki Deep Sea, Uwezeshaji wa kituo cha Tanga TV, Ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya English Medium, Kupima viwanja 500 kwenye maeneo ya Amboni, Tongoni, Mabokweni na Ndaoya. 

Aidha aliitaja miradi mengineyo kuwa ni Halmashauri hiyo imetenga fedha za uendeshaji wa ofisi za Kata na za Mitaa, ambapo kiasi cha shillingi Million 20 kitatolewa kila baada ya miezi mitatu katika kata zote 27, na kiasi cha shillingi 200,000.00 kimetengwa kutolewa kwa kila mtaa kwa kila robo mwaka.

Wakizungumzia bajeti hiyo madiwani wa Halmashauri hiyo kutoka kata mbalimbali Jijini Tanga walionekana kuridhishwa nayo kutokana na kuakisi maendeleo ya wananchi.

 Akizungumza bajeti hiyo Diwani Viti Maalumu katika Jiji hilo  (CCM) Mwanaidi Kombo alisema bejeti hiyo imepita kwa furaha kwa sababu imeongezeka karibia Bilioni 1 na vile vipaumbele vya wananchi  vimeanishwa ikiwemo suala la vijana,walemavu na masuala ya  miradi ya maendeleo

Alisema  pia ikiwemo miradi ya kimkakati ambayo imeingizwa kwenye bajeti hiyo na itakuwa chachu kwenye kuakisi maendeleo,masoko,hospitali,vituo vya afya  vimeingizwa jamboa ambalo ni muhimu kwa ustawi wa maendeleo.

Naye kwa upande wake  Diwani wa Kata ya Chongoleani (CCM) Mwaveso Mbega alisema bajeti hiyo imekidhi vigezo vinavyotajika kwa ajili ya maendeleo ya Jiji la Tanga kwa sababu imekusanya karibia vitu vyote vinavyohitaji kwenye maendeleo ikiwemo elimu,afya ,miundombinu ya b arabara,vijana wakina mama na walamevu.

Alisema ukiangalia bajeti ipo vizuri na wanaamini kutokana na mipango yao madiwani kwenye kusimamia ukusanyaji  wa mapato na serikali ni sikuvu yenye kuwajali watu wake na wana matumaini mafungu nafasi inayoichangia kuweza bajeti hiyo itakuja kwa ajili ya kukamilina na mambo yatakwenda vizuri.

 

 

 

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: