*********************

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam watumiaji wa huduma za usafiri ardhini(UNIFORUM-UDSM),wameliomba baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini(LATRA CCC) kuendelea kufungua majukwaa katika vyuo mbalimbali Nchini.

Hayo yamesemwa na Catherine Mkama Mwenyekiti wa Jukwaa la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam watumiaji wa huduma za usafiri ardhini katika zoezi la utoaji elimu na kuwakaribisha wanajukwaa wapya wa mwaka wa kwanza chuoni hapo, iliyofanyika leo Tarehe 22 Juni 2022 kwenye ukumbi wa Coet A 21 uliopo chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa jukwaa hilo la chuo kikuu cha Dar es Salaam limewasaidia kufahamu haki na wajibu watumiapo huduma za usafiri ardhini na limewajengea uwezo wa kuwa mabalozi wazuri kwa ngazi ya Jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla.

Kwa Upande wake Agness Stanley ambae ni mwanajukwaa mpya ameshukuru baraza kwa kuratibu zoezi zima na kuona kunaumuhimu wa uwepo wa majukwaa haya katika vyuo mbalimbali`'kwakweli leo nimeondoka na jambo hasa kwenye kulifahamu baraza,malengo na kufahamu umuhimu wa kutambua haki na wajibu nitumiapo vyombo vya usafiri ardhini."amesema Stanley.

Jukwaa hili lilizinduliwa rasmi Juni 26 2021 likiwa na lengo kubwa la kuwaongezea uwezo wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutambua haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za usafiri ardhini na kwa upande wa baraza utekelezaji wa mpango wa kuendelea kufungua majukwaa katika vyuo mbalimbali Nchini unaendelea kwa hivi karibuni mpango upo kuzindua Jukwaa katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: