Fedha zaidi ya sh. milioni 900 zilizotokana na uviko 19 zimesaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi jamii ya kifugaji wilayani Monduli mkoani Arusha kutembea umbali mrefu kufuata elimu hali iliyokuwa inasababisha baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo na wengine kupata ajali katika makorongo kwa kipindi cha msimu wa mvua.Akizungumza katika shule ya msingi shikizi Moita Krorit mbele ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ya mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya hiyo ,Frank Mwaisumbe alisema wilayani hapo walikuwa na hali mbaya ya uhaba wa madarasa kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wanakaa chini katika shule shikizi na wengine kusoma chini ya miti."Na baadhi ya madarasa yalikuwa ni tembe za udongo na zingine zilikuwa  hazijaezekwa kabisa lakini baadhi ya maeneo wanafunzi waliladhimika kutembea umbali mrefu takribani kilometa 44 kwenda shule na kurudi majumbani kwao,"alisema Mwaisumbe.
Aidha Mwaisumbe alisema  kipindi hicho watoto wengi walikuwa hawaendi shule na wengine ikiwabidi wazazi na walezi walikuwa wakiwaombea mahali pa kulala katika makazi yaliyokaribu na shule hivyo kulikuwa na umuhimu  kupata fedha hizo ikiwa juhudi za wilaya za kuchangishana ziligonga mwamba.Alisema juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na ukame ambao uliwakuta katika wilaya na nchi kwa ujumla hivyo ilifika mahali walikwama kutokana na wananchi kushindwa kuchangia kutokana na kutokuweza kufanya shughuli zao za kilimo na mifugo.Naye Afisa elimu mkoa wa Arusha,Abel Ntupwa,alisema fedha hizo zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu na uchumi hivyo anawahaidi kuwa walimu watalipa katika kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wanafunzi ikiwa ndio dhamira yao.Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Monduli ,Fredrick Lowasa alisema wao kama wanamonduli kuanzia Octoba 2021 na january 2022 wamepokea takribani sh.bilioni mbili hivyo wapo kwenye mchakato wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara ya Moita  kwenda Oljoro katika kusaidia kuinua uchumi wa halmashauri."Hivyo tunaomba JKT watusaidie kupata machimbo ya kokoto kwani  itaturahisishia gharama  kupungua na mimi nitajitahidi na tunaomba mtusaidie kwa hilo,"alisema.Katibu tawala mkoa wa Arusha,Athman Kihamia alisema kila halmashauri mkoani humo imeweza kupokea fedha takribani sh.milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya  za sekondari isipokuwa ngorongoro na Monduli wamepata takribani sh.milioni 940 kila moja  na zipo kwenye akaunti zao.Kihamia alisema shule hizo lazima wapate walimu pamoja na miundombinu ya vyoo lakini pia katika sekta ya afya pia kila halmashauri imepatiwa na serikali takribani sh.milioni 250 ikiwa lengo ni kukamilisha vituo vya afya."Na mnamo januari 10 tumepokea takribani sh.milioni 530 kwa ajili ya uboreshaji wa hospitali ya rufaa mountimeru ili kusaidia wgonjwa watakaopata rufaa katika hospitali za wilaya wakifika hospitalini hapo kila kiti wakione ni cha kisasa,"alisema Kihamia.Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Arusha,Zelote Stevene alisema lengo la serikali ni kuwaondoa maadui watatu wakiwemo umaskini,maradhi na ujinga na kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na maendeleo mbalimbali ya nchi."Wanaishukuru serikali kwa mkakati huu wa ujenzi wa madarasa pamoja na ukamilishaji wa vituo vya afya ambapo miradi hiyo imewagusa moja kwa moja wananchi na wengine kupata ajira hivyo zitaondoa kero zilizokuwa zinatukamili wakiwemo hawa adui watatu,"alisema Mwenyekiti Zelote.Nao baadhi ya wananchi waliofikiwa na miradi hiyo waliishukuru serikali kwani hapo awali watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule na wamama wajawazito walikuwa wanajifungulia njiani lakini sasa hivyo serikali imefanikiwa kuondoa changamoto hiyo.Hata kamati hiyo ilipanda miti katika shule ya sekondari Ilksongo pamoja na Mwenyekiti Zelote kutoa vyeti wa shule ziliwai kumaliza mradi wa madarasa kabla ya muda waliopangiwa na serikali kufika sambaba na kuzindua madarasa manne yaliyojengwa kwa fedha za uviko 19.

Share To:

Post A Comment: