Na. Angela Msimbira TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa leo amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ambaye .
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Rais - TAMISEMI iliyopo Sokoine Jijijini Dodoma ambapo Waziri Ummy ameishukuru Menejimenti na watumishi kwa ushirikiano walioonyesha kipindi alipokuwa akihudumu katika ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Inoncent Bashungwa amesema kuwa TAMISEMI si ngumu kama watumishi wote watajenga mahusiano bora na kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wakati, na kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi kwa kutoa huduma bora.
Waziri Bashungwa amewaagiza watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuendelea kushirikiana katika kufanyakazi kwa umoja na mshikamano kwa kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wanamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani katika kuwahudumia wananchi na taifa kwa ujumla.
Naye Waziri Ummy amesema kuwa TAMISEMI sio ngumu bali ni kubwa lakini ni kubwa kwakuwa inakupa uwanja mpana wa kuchagua jinsi gani utakavyoweza kufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine ili kukamilisha malengo yaliyopangwa kwa wakati huku kila mmoja akitimiza majukumu yake katika kutatua changamoto na kuboresha huduma katika jamii.
Amesema kuwa uongozi ni kushirikisha wengine ili waweze kujua muelekeo na maono ya kiongozi wao lengo likiwa ni kupata matokeo chanya katika utendaji kazi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuwataka watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa ushirikiano kwa Waziri Bashungwa ili kuweza kutimiza majukumu yake kikamilifu.
Wakati huohuo Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe. Devid Silinde amemshukuru Waziri Ummy kwa kufanyakazi kwa muda wa miezi tisa lakini ameacha alama isiyofutika kwa jamiia, ambayo ni ujenzi wa madarasa 15,000 ndani ya miezi miwili, kuongeza bajeti ya TARURA KU 273.5 hadi bilioni 966, ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali za Halmashauri.
Vilevile, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia afya Mhe Festo Dugange amemshukuru Waziri Ummy kwa kufanyakazi kwa pamoja na kuwa mmoja ya walioleta mabadiliko katika utendaji kazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ndani ya miezi 9 aliyohudumu.
Post A Comment: