Jeshi la polisi mkoa wa Manyara katika operesheni zao, wamegundua kiwanda bubu kilichopo kata ya Ngarenaro mjini Babati, kinachozalisha pombe kali feki zinazofungashwa kwenye vifungashio vya kampuni ya Konyagi.

Jeshi hilo limekamata shehena ya pombe hizo  feki huku wakiwaweka wafanyakazi wa kiwanda hicho chini ya ulinzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa manyara Benjamin Kuzaga akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa operesheni hiyo inalenga kuondoa bidhaa feki ambazo nihatarishi kwa afya ya binadamu na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho feki aliejulikana kwa jina babu moses amesikika akisema wanafanya kazi hiyo ili kujiingizia kipato na kwamba wanao usajili ambao hajauweka bayana.

Makamu mwenyekiti viwanda kutoka chama cha wafanyabiashara mkoa wa Manyara (TCCIA) David Mulokozi amesema kuwa uwepo wa viwanda bubu unaikosesha serikali mapato pamoja na kuathiri afya za watumiaji wa bidhaa hizo na kuisababishia serikali hasara kubwa kwa kuwa hawalipi kodi.

Pombe hizo feki zinaonekana zikiwa zimebandikwa stika zenye nembo ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambapo mtaani zinaingizwa zikiwa na jina la Konyagi.

Share To:

Post A Comment: