Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa mgodi huo kuhusu namna wanavyohifadhi na kutunza mazingira.

Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) walipofanya ziara katika mgodi wa North Mara kukagua utekelezaji wa Sheria ya mazingira katika mgodi huo.Baadhi ya wataalam toka NEMC waliotembelea mgodi wa North Mara na kupongeza juhudi zinazofanywa na mgodi huo za utunzaji wa mazingira. Mashine inayotumiwa na mgodi wa North Mara katika kuchakata maji taka kutoka kwenye mgodi huo.

****************

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka ameupongeza uongozi wa mgodi wa North Mara kwa kutekeleza kwa haraka maagizo waliowapatia kwa kupunguza maji ambayo yalikuwa yamezidi katika bwawa tope sumu(TSF) lililopo kwenye mgodi huo.

Ametoa pongezi hizo tarehe 22/01/2022 wakati akifanya ziara ya ukaguzi katika mgodi huo uliopo Tarime Mkoani Mara kuhakikisha mgodi huo unafuata taratibu kuondokana na uchafuzi wa mazingira.

"Ni jambo la kufurahisha kwamba kabla ya miezi sita ule muda ambao walitakiwa kufanya wameweza kuyasafisha maji yote yale ambayo yalikuwa ni machafu na yamesharudishwa kwenye mazingira". Amesema Dkt.Gwamaka.

Aidha Dkt.Gwamaka amesema ikiwa uongozi wa mgodi wa North Mara wataendelea na kasi ya kupunguza maji katika mgodi huo, uchafuzi wa maeneo hayo kwenye mazingira utapungua au kuisha kabisa.

Pamoja na hayo amewapongeza kwa kutengeneza mitaro ambayo itasaidia kuepusha kujaa maji katika mgodi huo.

Naye mmoja wa viongozi katika mgodi wa North Mara Bw.Majuto Kapande amesema Serikali kupitia NEMC wamekuwa wakiwapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanathibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo yya mgodi ambapo mpaka sasa wamekuwa wakitekeleza maagizo yanayotolewa na NEMC kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.

"Bwawa letu la TSF lilikuwa na maji kiasi cha mita za ujazo milioni 7 ambazo zinazidi kiwango kinachotakiwa cha mita za ujazo laki 8. NEMC kwa kushirikiana na Wizara ya Maji walikuja na kutuelezea ni namna gani tunaweza kupunguza maji katika bwawa la TSF na sasa bwawa lina maji ambayo yanatakiwa kulingana na design chini ya laki 8". Amesema Bw.Kapande.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: