Na Mwandishi Wetu.

 Ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwa kampeni  ya WAJIFTISHE GIFTI JUU YA GIFTI inayoendeshwa  na Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania, Bibi  Frola Willison Rutabingwa ameibuka mshindi wa pikipiki aina ya Boxer kupitia KAMPENI YA TIGO "WAGIFTISHE  GIFT JUU YA GIFT" baada ya kununuliwa  simu katika duka la Tigo.

Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa pikipiki mshindi huyo ameishukuru Tigo kwa kuwajali wateja wake na kuamua kurudisha kwa wateja kupitia zawadi.

"Nilinunuliwa simu ya Shilingi elfu 89 katika duka la Tigo  na Mume wangu kipenzi hatimae baada ya muda Nilipigiwa simu na Tigo kuwa nimeshinda pikipiki nawashukuru Tigo mmesongesha maisha yangu lakini pia namshukuru Mume wangu kwa upendo wake". Alisema  Bi. Frola  Mshindi wa Pikipiki.Akimpongeza na kukabidhi zawadi kwa mshindi wa pikipiki hiyo pamoja na washindi waliojishindia simu janja Meneja wa Mauzo  Tigo Buharamulo , Bwana Aman Sailoja  amesema katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, kampuni ya Tigo imewahakikishia wateja wake kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, hivyo akawaomba wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 na simu nyingine kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki  zikiwemo simu janja zinawaniwa katika promosheni hiyo.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: