Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania, Heri Rashid wakipanda mche wa mti wakati akizindua zoezi la upandaji miti iliyotolewa na Taasisi hiyo katika Kijiji cha Munkhola Kata ya Mgori wilayani humo ambapo miche ya miti 3000 inatarajiwa kupandwa kwenye maeneo ya misitu.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri (kushoto) akikabidhiwa mche wa mti na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania,  Heri Rashid  wakati wa uzinduzi huo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania,  Heri Rashid  akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Singida, William Nyalandu akizungumza kwenye uzinduzi huo.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Muhifadhi wa Misitu  Wilaya ya Singida, Uswege Mwasumbi akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo mkoani hapa  Ibrahim Mghama akisoma risala kwenye uzinduzi huo.Burudani zikitolewa kwenye uzinduzi huo.

Diwani wa Kata ya Mgori  Dhuma Said akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Burudani zikiendelea.
Wadau wa misitu wakiserebuka wakati wa uzinduzi huo.
Miche ya miti ikishushwa kwenye gari.
Safari ya kwenda kupanda miche hiyo ya miti ikifanyika.
Utambulisho wa viongozi ukifanyika kwenye uzinduzi huo.
Katibu Tarafa ya Mgori, Bornege Tatwebwa akizungumza.
Wanawake wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Munkhola Ramadhan Mambue akizungumza.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mgori Julieth Mchawa akizungumza.


Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi na kutoa salamu ukiendelea.
Diwani wa Kata ya Merya Iddi Kijida akizungumza.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.

Uzinduzi ukiendelea.
Mkazi wa Kata ya Mgori Asia Salim akipanda mche wa mti kwenye uzinduzi huo.
Muhifadhi wa Misitu  Wilaya ya Singida, Uswege Mwasumbi akipanda mche wa mti.
Muonekano wa eneo lililopandwa miche ya miti.


 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

MKUU wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wananchi waliovamia na kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na uchomaji mkaa kwenye misitu ya Munkhola na Mgori ili kudhibiti uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika kwenye misitu hiyo.

Muragili alitoa agizo hilo wakati akizindua zoezi la upandaji miti iliyotolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania katika Kijiji cha Munkhola Kata ya Mgori wilaya humo ambapo miche ya miti 3000 inatarajiwa kupandwa kwenye maeneo hayo ya misitu.

"Wale wote walioenda kulima kwenye maeneo hayo wakamatwe kwani tunawajua hatuwezi kulinda misitu yetu lakini watu wachache wanaendelea kuhalibu, najua mnamahitaji makubwa ya chakula lakini hatuwezi kuhalibu mazingira kwa gharama ya chakula ili jambo haliwekani" alisema Muragili.

Muragili alisema kila mtu wilayani humo ana wajibu wa kuitunza misitu na akatumia nafasi hiyo kuipongeza Taasisi ya Trees for the Future Tanzania kwa jitihada zake inazozifanya za kuisaidia Serikali katika utunzaji wa mazingira.

Katika hatua nyingine Muragili ameagiza kila kaya katika wilaya hiyo ihakikishe inalima ekari isiyo pungua moja ya zao la mtama ili kukabiliana na uhaba wa chakula ambao utaweza kutokea  kutokana na ukosefu wa mvua.

"Ili ni agizo watendaji na viongozi wote wa halmashauri nitafanya ukaguzi wa kaya hadi kaya na kaya ambayo itakutwa haijalima mtama tuaiadhibu ni lazima tuwe na zao la tahadhari ikitokea bahati mbaya neema ya Mungu haijatushukia hatujapata mvua mpaka mwezi wa tano na ikatokea bahati mbaya mazao ya mahindi tukayakosa basi mtama liwe zao la kutuokoa" alisema Muragili.

Mragili aliwashauri wananchi hao kupanda mazao mengine yanayotumia maji kidogo jambo litakalosaidia kupata chakula badala ya kusubiria kulima mazao yanayotumia maji mengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Heri Rashid alisema taasisi hiyo inajihusisha na uhamasishaji  wa kilimo endelevu kwa kutumia miti huku wakiamini kuwa miti ndio vyanzo vizuri vya maisha na vipo katika mazingira.

Alisema mazingira yanaharibiwa sana kutokana na shughuli za kibinadamu kama kukata miti kwa ajili  kilimo, kujengea,malisho ya mifugo na shughuli mbalimbali imepelekea maeneo mengi kuwa wazi na kuharibu uoto wa asili hivyo wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Singida kama juhudi zao za kuhamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi ili waweze kurudisha uoto wa asili na hali ya hewa kurudi katika hali yake ya kawaida.

Alisema miaka ya nyuma Singida ilikuwa na mvua za kutosha na vyanzo vya maji vilikuwa vingilakini sasa hali hiyo haipo tena ndio maana Taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kuhamasisha upandaji wa miti.

Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo mkoani hapa  Ibrahim Mghama alisema katika kutekeleza malengo yake ya kupanda miti, inawawezesha kifedha wadau wa maendeleo mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za za upandaji miti na uhifadhi wa mazingira nchini ikiwemo Magereza Tanzania kupitia Gereza la Uyui-Tabora, Ilagala-Kigoma, Msalato-Dodoma, Manyoni-Singida na Gereza la Shinyanga.

Aidha alisema taasisi hiyo inasaidia asasi za kiraia zinazofanyakazi na wakulima ambazo ni ADESE

na WAENDELEE za Mkoa wa Singida, TaDeCaO na Frontie Friends of Environment za Mkoa wa Tabora, Women Against Poverty ya Mkoa wa Dar es Salaam, Twitange ya Mkoa wa Iringa, Environment Develepment Group na Life Securing and Relief Services za Mkoa wa Shinyanga na Friends of Lake Tanganyika ya Mkoa wa Kigoma na kuwa kwa kipee taasisi hiyo inashirikiana na Clinton Development Initiative (CDI) iliyoko Mkoa wa Iringa na HELVETAS ya Singida.

Alisema katika Mkoa wa Singida wanafanya kazi katika Halmashauri nne ambazo ni Ikungi, Iramba, Mkalama na Singida.

Alisema katika tukio la leo wamepanga kupanda miche ya miti 3,000 katika msitu wa Munkhola na kugawa kwa wananchi wanaouzunguka msitu huo miche ya miti 2,000 na kuwa lengo la mwaka huu nikupanda miti 2,466,300 iliyozalishwa na washirika na wakulima wa Wilaya ya Singida kwa  ujumla.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: