Na Asila Twaha, TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt. Grace Magembe amewataka wataalam wa afya na wadau kushirikiana  kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Selimundu(Sickle Cell).


Dkt.Grace amesema hayo Desemba 7,  2021 Jijini Dodoma wakati akipokea ripoti ya Tanzania Sickle Cell Disease Alliance (TANSCDA) iliyoeleza  jinsi  ilivyotoa elimu ya upimaji na jinsi ya kujikinga  juu ya ugonjwa wa selimundu  katika mashule  na vyuo  Tanzania.


Amesema pamoja na takwimu kuonesha Tanzania jumla ya watoto 11,000 kila mwaka wanazaliwa na ugonjwa wa selimundu na  kwa upande wa  Mikoa ya Kanda ya Ziwa  na Pwani tatizo ni kubwa, amewataka wataalam  wa afya kuhakikisha kunakuwepo na  mashine zitakazo tambua mgonjwa mwenye vinasaba vya selimundu(Sickle Cell) mapema ili kusaidia kupata matibabu kwa haraka.


“kwenye masuala ya kuangalia afya ya jamii hatuangalii gharama ndio mana kuna gharama Serikali hua inazibeba sababu suala hili linagusa afya ya kila mtanzania” amesema Dkt. Grace


Ametoa wito kwa jamii kuto wanyanyapaa  wagonjwa wa selimundu na kuwataka wataalam na wadau kutumia njia rahisi ya mawasiliano ambayo itatoa ujumbe na elimu kwa jamii  juu ya ungonjwa wa selimundu.


“Ni vizuri pia kuwapatia elimu viongozi wetu wa dini na kimila wa kijua elimu kuhusu ugonjwa wa selimundu ni vizuri  itasaidia  wao  kutoa sababu  asilimia kubwa ndoa zinafungwa kanisani na msikitini  wakijua hii elimu watatusaidia kuitoa kwa jamii” amesisitiza Dkt. Grace


Mtendaji Mkuu, Tanzania Sickle Cell Disease Alliance (TANSCDA) Dkt. Deogratias Soka ameishukuru Serikali na kuiomba kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii.

Share To:

Post A Comment: