Na Woinde Shizza Arusha,


Zaidi ya tani 30. 8 za madini aina ya  Ruby yenye thamani ya shilingi bilioni 3,165,208,679.80 yamechimbwa katika Mgodi wa Sendeu Agrovet Co. Ltd uliopo wilayanu  Longido Mkoani Arusha.


Jumla ya tani 178.495 za madini yamechimbwa na kufanyiwa uthaminishaji na kubainisha thamani ya madini yaliyochimbwa katika mgodi huo ulioanza uzalishaji Mwaka 2019 kuwa ni shilingi 5,791,347,239.63 hadi kufikia 5 Novemba  5 ,mwaka huu 2021.


Hayo yamebainishwa na mmiliki wa mgodi wa Sendeu Agrovet co.ltd Sendeu Laiza wakati akiongea na waandishi wa habari wakati waziri wa  madini Doto Biteko  alipotembelea mgodi huo nakuona jinsi wanavyoendesha shughuli zao.


Alibainisha kuwa uchimbaju rasmi wa madini ya Ruby katika Kijiji cha mundarara ulianza mwaka 1948 na ulianza kufanywa na kampuni ya kigeni iliokuwa imesajiliwa nchini Kenya iliojulika Kwa jina la Continental Ore Company ltd.


Sendeu alisema baada ya Tanganyika kupata Uhuru mwaka 1961 serikali ya Tanzania iliutaifisha mgodi huo mnamo mwaka 1973 na kukabidhiwa Kwa Tanzania Gemstone industries ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la madini la taifa (STAMICO).


Alisema  kuwa tangu kukabidhiwa Kwa mgodi huo kwa kampuni yake   mwaka 2009 zaidi ya tani 30.8 za madini ya Ruby yamechibwa  katika mgodi huo na jumla ya tani178.495 yamechibwa  nakufanyiwa uthaminishaji na kubainishwa thamani ya madini yake.Akiongea mara baada ya kutembelea mgodi huo waziri wa Madini, Doto Biteko  ameipongeza kampuni ya Sendeu Agrovet Co. Ltd kwa kupata madini hayo na kuwataka wachimbaji wa Madini ya Ruby kupendana, kuheshimiana na kuthaminiana.


Alisema kuwa mahali popote penye ridhiki hapakosi migogoro, hivyo alimuomba  Sendeu  akae vizuri na watu wasigombane  bali waheshimiane na wathaminiane kwani  Rais  wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia   Suluhu anataka kuona wachimbaji wanatajirika


Biteko alisema Serikali itaendelea kumuunga mkono mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa Ruby Sendeu Laiza na kumtaka achimbe kwa kufuata Sheria na kuzingatia kulipa kodi za Serikali.


Aidha, alibainisha  uwepo wa madini ya rudy katika kijiji cha Mundarara ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa Mundarara, wilaya ya Longido na kwa watanzania wote kwa ujumla.


Biteko alitoa wito kwa wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na wadau wote kuendelea kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ili kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na stahiki ya Serikali.

Share To:

Post A Comment: