Na.WAMJW-Arusha


Serikali ina nia njema na kuwatakia afya njema wananchi wake ili waendelee kuzalisha na kuwa  na uchumi  mzuri.


Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu ,Wizara ya afya Prof.Abel  Makubi wakati akiongea na wenyeviti wa serikali mtaa, vitongoji ,kidini , kamati ya ulinzi na Usalama na viongozi wengine katika kuelekea  kwenye uzinduzi wa awamu ya pili wa mpango shirikishi na harakishi wa uhamasishji wa chanjo dhidi ya Uviko-19, itakayofanyika 22/12/2021.


Prof. Makubi amesema kuwa Serikali chini ya Rais Samia Sulluhu Hassan ina nia njema kwa wananchi wake na hivyo kuhakikisha Wananchi wanapata kinga na hivyo kufikia asilimia 60 ya kinga kwa muda mfupi. 


"Hakuna chanjo iliyofanikiwa kwa kulazimisha bali kwa kuelimishana na wananchi na kuelewa sayansi , hivyo baadae mtu kuamua kuchanja Kwa hiari yake. 


Aidha,Amesema kampeni hiyo ambayo itaenda  kuwatumia viongozi wa mitaa wenyewe ,"lazima mlimiliki na mlifanye ninyi wenyewe na ndio maana tumeamua kushusha kwa wananchi na wote kuwa timu moja  mtaani".


Aidha,Prof. Makubi amefafanua, Kampeni ya mtaa Kwa mtaa, haileti ulazima bali ni kupeana elimu ngazi ya mtaa na Wananchi kwa hiari yao kwenda kuchanja .


Hata hivyo Prof. Makubi alisema licha ya kuchanja bado wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono mara kwa mara na maji tiririka na sabuni,kuepuka misongamano na kuvaa barakoa.


"Jambo jingine niwakumbushe wananchi kufanya mazoezi pamoja na kula lishe bora,kwani mazoezi ni muhimu na inasaidia mifumo ya hewa kuwa mizuri"Alisisitiza Prof.Makubi


Naye, Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa nchi inapoelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka wameona ni muhimu kushirikishana na viongozi wa dini,mitaa na kimila ili kuwa na namna bora ya kuwafikia wananchi ili kuweza kuwalinda wazee waliopo majumbani.


Prof.Shemdoe hakusita kuwakumbusha viongozi hao kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19  na kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

Share To:

Post A Comment: