Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile Ameungana na Mamia ya Waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mjini Kasulu Mkoani Kigoma kusali Misa Takatifu ya Krismasi ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. 


Baada ya Misa hiyo iliyoongozwa na Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya western Tanganyika Sadock Makaya, Mbunge Ditopile amewapongeza na kuwatakia heri watanzania wote kwa sikukuu ya Krismasi na kuendelea kumshukuru Mungu kwa Miujiza na upendo mkubwa analolitendea Taifa la Tanzania.


Akizungumza kwa Niaba ya Waumini, Askofu Sadock Makaya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna anaongoza Taifa kwa weredi, Busara na Upendo mkubwa 


"Ndugu waumini wenzangu Taifa letu limepata bahati kubwa ya kupata Rais Mwanamke, ambaye ni Mchapakazi, Mwadilifu, ana upendo mkubwa kwa watu wote analipeleka Taifa letu mbele kwa kasi kubwa, tuendelee kumuombea na tumuunge mkono" 


Askofu Sadock Pia amesema   Tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie Madarakani ndani ya muda mguamefanikisha kutatua baadhi ya Masuala yalikuwa yakilitatiza Dayosisi hiyo kwa muda mrefu. 


Askofu Sadock amesema Kanisa hilo linamuunga Mkono Rais Samia kwa vitendo na tayari  Kanisa limeanza ujenzi wa kiwanda cha ujasiriamali ambacho kitatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 800 na Vibarua 1500. Kiwanda Hicho kinajengwa na Kanisa hilo Mjini Kasulu chini ya Ufadhili wa Serikali ya Ujerumani.

Share To:

Post A Comment: