Taasisi isiyo ya kiserikali ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF) imeandaa mafunzo kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo ili kuwajengea uwezo waweze kuboresha biashara zao ili kuziongezea thamani.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Maryprisca ambaye ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya amesema lengo la taasisi  ni kuwaunganisha wanawake katika vikundi waweze kuzitumia pia fursa za mikopo inayotolewa katika halmashauri.


Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka VETA Morogoro Sophia Tuka amewataka wanawake kutulia na biashara moja na kuwataka kutunza raslimali.


Sophia ameshauri wajasiriamali kuwa na daftari la mapato na matumizi.

Share To:

Post A Comment: