Na Jane Edward,Arusha 

TIMU za mpira wa miguu za Bunge la  Zanzibar pamoja na Kenya zimeanza vizuri mashindano ya mabunge wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea kutimua  vumbi  viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid  yanayoendelea baada ya kushinda mechi zao za kwanza 

Timu hizo ambazo zimechezwa  leo ambapo timu ya Zanzibar ilibahatika kuibuka naushindi wa bao 2 kwa 0 dhidi ya timu ya Uganda,kwa upande wa timu ya bunge la Kenya imeweza kufunga  bao moja kwa 0 lililofungwa kwa mkwaju   wa penati  lililoingizwa nyavuni na Senetar Kipchumba Murkomen kunako dakika ya 76 ambapo penati hiyo ilisababishwa na mchezaji wa timu ya Bunge la Jumuiya alietambulika kwa jina la John  kibwana mara baada kuunawa mpira katika eneo la penati

Kwa upande wa timu za netiboli za Bunge la Tanzania na bingwa Uganda zimeanza vyema mashindano ya Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Mechi hizo zilichezwa ambapo  bingwa mtetezi Uganda iliifundisha Kenya Netiboli inatakiwa kuchezwa vipi baada ya kuikung’uta magoli 53 kwa 5 na kuonyesha nia ya kutaka kutetea tena ubingwa wao huku mchezo wa pili Tanzania wakiwatandika wageni wa michuano hiyo baraza la wawakilishi Zanzibar 44 kwa 32.

Kocha wa timu ya Bunge la Tanzania,Daniel Nchonya alisema mchezo huo ni moja kati ya kutimiza azma yao ya kutaka kutwaa ubingwa kwani wamejipanga vyema kuhakikisha kombe lina baki na siyo kutoka nje ya nchi.

Alisema uwepo wa wabunge wengi vijana katika kikosi chake inampa matumaini ya kuendelea kufanya vizuri kwani wanajituma lakini pia wanafanyia kazi maelekezo yote ambayo anawapa huku akiwataka watanzania kuwa na imani na timu yao kwani ni nzuri na wamedhamiria kufanya kweli.

“Tumejipanga ingawa wanasema ni dakika 60 za netiboli lakini sioni kama kuna timu itatunyima nafasi ya kutwaa ubingwa tuko vizuri na vijana morali yao iko juu”alisema Nchonya.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Bunge la Uganda,Mugerwa Fred alisema baada ya ushindi dhidi ya Kenya sasa wanaenda kujipanga vyema kuhakikisha wanashinda na mchezo unaofuata kwani mikakati yake ni kutetea tena taji lao na anaamini hilo litawezekana kutokana na namna walivyojipanga.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Mechi hizo mbunge wa Bunge la Tanzania kutoka Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete alipongeza timu ya Bunge la Zanzibar kwa kuanza vyema mashindano hayo japo kuwa timu hiyo ndio mara yao ya Kwanza kushiriki na kubainishwa kuwa matokeo ya leo yanawapa motisha zaidi ya kuonyesha timu hiyo ipo vyema  inajiamini

Alisema kuwa kuwa  wao Kama timu ya Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wanatarajia kucheza kesho na kubainishwa kuwa watahakikisha wanacheza vyema na kupata ushindi wakishindo ambao utawafurahisha watanzania na kuiheshimisha nchi na wananchi wote kwa ujumla.

Ikumbukwe kuwa michezo hiyo ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika mashariki imeandaliwa na bunge la jumuiya ya Afrika mashariki kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu na mabunge hayo kuelekea kilele cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.

Share To:

Post A Comment: