Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora wamefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa ya Sekondari 87 ambavyo vimegharimu shilingi Bil 1.74 fedha kutoka kwenye Mradi wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.


Fedha walizozipata mwezi October,2021 zimefanikisha ujenzi wa vyumba 87 ambavyo vimekamilika na vitawezesha asilimia 56 ya wanafunzi  waliofauli darasa la saba kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja.


Akiwa ziarani Wilayani humo Mhe. Ummy Mwalimu amekagua madarasa matatu yaliyojengwa kwenye shule ya Sekondari Kampala kwa niana ya madarasa yote 87 yaliyojengwa katika Halmashauri hiyo.


Mhe. Ummy ameridhwa na ubora wa vyumba hivyo vya madarasa na amewapongeza kwa usimamizi makini uliofanikisha ukamilishaji wa vyumba vya madarasa hayo. 


Kwa upande wa Vituo shikizi Halmashauri ya Wilaya ya Nzega walipata shilingi Milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 29 kwenye vituo shikizi.

Share To:

Post A Comment: