MKURUGENZI wa Taasisi ya Ebenezer English Medium Primary School za Jijini Tanga Issack Mlangwa akizungumza na waandishi wa habari

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MKURUGENZI wa Taasisi ya Ebenezer English Medium Primary School za Jijini Tanga Issack Mlangwa amempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuboresha sekta ya elimu hapa nchini ikiwemo kutoa ajira kwa walimu kutokana na mahitaji yaliyopo tokea aingie madarakani

Pongezi hiyo alilizitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya darasa la saba yaliyotoka hivi karibuni ambapo shule ya Msingi ya Ebenezer English Medium Primary School iliweza kuongeza kiwilaya na kimkoa kwa kushikaa nafasi ya kwanza.

Shule hiyo iliibuka kinara wa matokeo ya darasa la saba kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2016 mpaka mwaka 2021 kiwilaya na mkoa wa Tanga huku walipania kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri ikiwemo kuibuka na kidedea kwenye ngazi ya Taifa kipindi kijacho.

Alisema wanasifu juhudi hizo kutokana na awali kulikuwa na uhaba wa walimu huku akimshauri  Rais kutoa nafasi nyingi na kuunga mkono wawekezaji katika sekta ya elimu  kwenye shule wa watu binafasi ili watoto wa kitanzania waweze kupata elimu bora .

“Kutokana na kwamba Serikali pekee haiwezi kwa hiyo zinahitajika za juhudi za makusudi ziweze kufanyika ili wawekezaji wengi waliopo kwenye sekta hiyo ili kuweza kuinua ubora mzuri.

Ambapo alisema kwa sababu Serikali pekee haiwezi kusimamia elimu hivyo juhudi za makusudi zinahitaji ili kuwasaidia wawekezaji wengi waliopo kwenye sekta hiyo ili kuweza kuleta ushindani nchini.

Mkurugenzi huyo alisema juhudi hizo zinatakiwa kufanyika ili kuweza kuvutia wawekezaji wengi ambao watachangia ushindani  na hivyo kusaidia kukuza ubora wa elimu.

Akizungumzia siri ya kuongoza kimkoa kila mwaka Mkurugenzi huyo alisema kikubwa ni ushirikiano kati ya walimu,wanafunzi,wazazi na utawala wa shule hiyo.

Alisema pili ni uongozi wa shule hiyo unajitahidi kumaliza mitaala mapema ili kuweza kupata muda wa kufanya marudio mara kwa mara na kufanya mitihani mingi kwa wiki wanafanya mitihani mitatu kwa kufanya marudi mara kwa mara.

Aidha alisema pia kuimarisha misingi ya nidhamu kwa walimu na wanafunzi ambao wanahudumiwa huku akielezea program yao ya masomo ya usiku kwa wale wanaokaa bwenini na wakishapata chakula chao wanapata masomo ya ziada hatua ambayo imeleta mafanikio chanya kwenye shule yao.

Alisema pia wanajisikia fahari kwa mafanikio wanayo pata kila siku lakini sio kubahatisha ni uwezo wa Mwenyezi Mungu ikiwemo baadhi ya walimu na wanafunzi wanajiwekea malengo na mikakati wanaojiwekea na walimu wao kwa ajili ya kupata matokeo.

“Mafanikio hayo yamechangia kutokana na walimu waliona waliobobea kwenye ufundishaji na wafanyakazi ambao wanatimiza wajibu wapo  na wanaamini mafanikio yao yanakuja na umoja na ushirikiana wao”Alisema

Awali akizungumza Mwalimu wa Shule ya Msingi Ebenezer Lucy Materu alisema wanajitahidi kuwa fundisha watoto kwa bidii lakini wanafanya mazoezi ya kutosha ambayo yanawezesha kufanya marudio vitu ambavyo wamefundishwa na walimu wao darasani hatua inayosaidia kwenye ufaulu wao.

Naye kwa upande wake Mwalimu Shamuni Hassani wa shule hiyo alisema matokeo ambayo wameyapata wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata matokeo hayo na jambo la kufurahisi kutokana na maandalizi waliyokuwa wameyafanya.

Akionekana kuunga mkono hoja hiyo Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Indian Ocean ya Jijini Tanga Judith Kimbute alisema jambo ambalo angeliomba Serikali iwafikirie shule binafsi kutokana na kwamba wana mchango mkubwa kwa serikali kusaidia jamii na wazazi wengine ambao hali zao zipo chini .

Alisema lakini wakati mwengine wanapambana nao huku wengine hawalipi ada zao kutokana na hali mbaya na kila mwaka wana madeni hatua ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma.

Mkurugenzi huyo aliiomba Serikali iwafikirie kwamba hao wanaoendesha shule binafsi wafanyiwe kitu kidogo ili waweze kuwasaidia ili nao waendelee na kuona kwamba serikali yao imewasaidia kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kukuza elimu nchini.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: