| MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira | 
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira ametimiza mwaka mmoja tokea alivyoapa tarehe 11 Novemba 2020 kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiwashukuru Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia Mkoa wake wa Kagera hadi Taifa na Wanawake wa Mkoa wa Kagera na Mikoa yote 32 Nchini kwa kumpa nafasi hiyo muhimu.
Aliyasema
 hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Novemba
 11,2021 ambapo alisema katika kipindi chake cha mwaka mmoja tokea amekuwa 
Mbunge amejikita zaidi katika maeneo nane ya kimkakati ikiwemo Lishe 
hususani shuleni, Sekta ya Kidigitali kwa maana ya umuhimu wa Serikali 
kuandaa Digitali Economy Strategy.
Mbunge
 Neema alisema eneo lingine ni kuhususu Diaspora ambapo Serikali iweke 
mazingira wezeshi ili watanzania wanaoishi nje ya nchi waweze kuwekeza 
na kuchangia Maendeleo ya Taifa lao kupitia Special Status yaani Hadhi 
Maalum 
Jambo jingine ni kupunguza msongamano kwenye magereza kwa kutafuta namna ya kupunguza idadi ya mahabusu.
Alisema
 pia suala lingine ni uhitaji na umuhimu mkubwa wa upatikanaji wa Taulo 
za Kike kwa Wanafunzi ambapo kwa mwaka huu 2021 ameweza kutoa msaada wa 
Taulo za Kike za Kutosha Mwaka Mzima kwa Wanafunzi 5,500 kutoka Mikoa 19
 Nchini kwa lengo la kuondosha changamoto ya kukosa shule kila mwezi 
wakiwa katika Hedhi. 
“Lakini
 pia umuhimu wa Mahakama ya Familia ili kuweza kuleta haki kwa uharaka 
zaidi kwenye maeneo ya mirathi na matunzo na kuendeleza mapambano ya 
kutokomeza malaria na magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipamble” Alisema
Hata
 hivyo pia alisema katika kipindi hicho suala lingine ni utambuzi wa 
mchango mkubwa wa Sekta ya Asasi za Kiraia (NGOs) kwenye Maendeleo ya 
Taifa na hapo wamefanikiwa kufanya Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la 
Taifa la NGOs (NACONGO) na kuandaa Mkutano wa Mwaka wa NGOs ambapo Rais 
Samia Suluhu Hassan alikuwa Mgeni Rasmi.
“Kwa
 nafasi ya kipekee namshukuru Mhe Job Ndugai, kwa namna anayotujengea 
uwezo na maarifa ili wao Wabunge ili tuendelee kuishauri vizuri Serikali
 “Alisema Mbunge Neema Lugangira.
Aidha,
 Mbunge Neema Lugangira alimpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa 
namna anavyongoza nchi na kuleta maendeleo  na yeye kama Mbunge anapata 
hamasa kubwa ya kuendelea kuishauri Serikali na kuchangia katika 
Maendeleo ya Taifa letu.
- MWISHO -

Post A Comment: