Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakary Kunenge akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Zainab Abdallah akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii wa Taarabu Isha mashauzi akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii wa kizazi kipya Ruby akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Mchekeshaji Nalimi Joseph akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii wa Singeli nchini Dulla Makabila akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii wa kizazi kipya Rapcha akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii Mrisho Mpoto akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. Msanii wa Singeli nchini Dulla Makabila akizungumza wakati wa utoaji taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

Wasanii na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika Tamasha la Kimataifa la Tamaduni na Sanaa Bagamoyo ambapo wasanii hao watatoa burudani.

Tamasha hilo ambalo ni la aina yake litafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 28 hadi Oktoba 30, 2021 katika Viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara itahakikisha tamasha hilo kuendelea kuwa kubwa na iwe sehemu ambayo vitu vyote vya asili vipatikana.

Amesema malengo ya Wizara kuendeleza, kuzikuza na kuzifanya sekta za sanaa na tamaduni ziweze kuwa na mchango mkubwa.

"Tamasha hili la Bagamoyo tutaliunganisha na maeneo yakutangaza utalii kutakuwa na tour mbalimbali za watu kwenda kwenye utalii lakini kuna siku moja ambapo ni tarehe 30 wasanii watatembelea Saadani". Amesema

Aidha Dkt.Abassi amesema nje ya kuwepo kwa burudani kutoka kwa wasanii kutakuwa pia na maonesho mbalimbali ya sanaa kutakuwa na vyakula vya kiutamaduni na vitu vingine vya asili.

Amesema kutakuwa na kila aina ya sanaa kama vile maigizo,Uchoraji, Uchongaji, Sarakasi pia kutakuwa na wasanii ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika tasnia hiyo wataweza kutoa burudani za kutosha.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakary Kunenge amesewahakikishia washiriki katika tamasha hilo usalama na amani katika kipindi chote cha tamasha hilo litakapokuwa linafanyika.

Amesema wamejipanga vizuri kwani tukio hilo litakuwa ni miongoni mwa matukio makubwa ya kihistoria na kutazidi kutangaza nchi yetu hasa wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: