Mkurugenzi Mtendaji Maji Safi na Mazingira  (SUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Patrick Nzamba (kushoto) akimuonesha Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge tenki la kuchanganyia 'chlorine powder' ambayo hutumika kutibu maji endapo umeme unakuwa umekatika. Kawaida SUWASA hutibu Maji kwa kutumia gesi ya klorini.
Ukaguzi wa miradi ya maji ukiendelea.
Mkuu wa mkoa alipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji SUWASA Mhandisi Patrick Nzamba.
Wageni walioambatana na Mkuu wa mkoa walipotembelea chanzo cha maji Mwankoko katika kituo cha kusukuma maji.
Mkuu wa mkoa pamoja na msafara wake wakielekea visimani Mwankoko.
Tanki la juu la Mandewa lenye lita 500,000 linalopokea maji kutoka chanzo cha maji Mwankoko. Pembeni ni tenki la chini lenye ujazo wa Lita milioni 2.5
Tenki la Somoku linavyoonekana na mradi wake umefikia 90%. Mradi huo una gharama ya milioni 755 ambapo kuna shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa tenki hilo, kulaza mtandao 13km kuunganisha wateja 500 na manunuzi ya pampu.

 
Na Mwandishi Wetu, Singida


MAMLAKA  ya Maji Safi na Mazingira Mkoa wa Singida (SUWASA) wametakiwa kutumia mbinu mbadala kuongeza ukusanyaji wa mapato ili waweze kuendeleza miundombinu na kupunguza upotevu wa maji.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati akizungumza na watumishi wa  SUWASA  baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji iliyojengwa na mamlaka hiyo.

 "Ukusanyaji wa mapato ukisimamiwa vizuri utasaidia kuongeza mapato na kukarabati miundombinu na usambazaji wa maji maeneo mengi zaidi kwa kutumia fedha za ndani,". alisema Mahenge.

Aidha Dkt. Mahenge amebainisha kwamba kiasi cha maji yanayopotea kwa Mkoa wa Singida ni asilimia 33.4 ambayo ni kiasi kikubwa kikilinganishwa na asilimia 22 ya upotevu inayokubalika hivyo kuwataka SUWASA kuhakikisha upotevu unapungua.

Hata hivyo Dkt. Mahenge ameipongeza SUWASA kwa kuanzisha miradi mingi ya maji ambayo imejengwa kwa kutumia fedha za ndani na kwa viwango vinavyokubalika .

RC ameishukuru serikali kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 3.07 ili kutekeleza miradi ya maji iliyopo Manispaa ya Singida, Wilaya ya Iramba na Ikungi Nawapongeza sana kwa kazi nzuri milofanya Miradi mingi iliyojengwa ina viwango vinavyokubalika kwa fedha za ndani hii inaonesha ubunifu mkubwa mliutumia katika kutekeleza miradi hii, niwaombe muendelee kusimamia vizuri makusanyo ili muweze kuanzisha miradi mingine, alisema Dkt. Mahenge.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wote mkoani hapo wanaotumia huduma ya maji kuhakikisha wanalipia huduma hiyo kwa wakati ili kusaidia Mamalaka kuendelea kusambaza huduma kwa watu wengine .

Naomba muandae orodha ya Taasisi na watu wote wanao daiwa nizipate ofsini kwangu,
lazima mtu aliyepatiwa huduma ya maji na akayatumia alipe, nitoe wito kwa yeyoteanayejua kwamba ana deni la maji alipe kabla orodha hiyo haijanifikia, alisisitiza Mahenge.

RC Mahenge amewakumbusha watumishi wa SUWASA kuhakikisha kwamba hakuna udanganyifu unaofanyika katika usomaji wa mita na kuacha ukadiriaji kwa mteja.Akimalizia hotuba yake Dkt. Mahenge amewaagiza watumishi kufanya ukaguzi wa kawaida utakaobaini ubora wa maji katika visima binafsi vinatoa huduma kwa wananchi na kuyapima ili kulinda afya za watu.

Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na mazingira Mkoani Singida (SUWASA) Mhandisi Patrick Nzamba amesema mkoani hapo wametekeleza jumla ya miradi ya maji saba 7 inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.075 katika Kata za Unyambwa, Minga, Mungu maji na Vijiji vya Misigiri na Ulemo.

Aidha amebinisha kwamba Mamlaka ina mpango wa kuongeza uzalishaji wa maji kwakuchimba visima 11 kupitia fedha za miradi 28 ya maji lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wengi wanapata maji.

Mhandisi Patrick amefafanua kwamba SUWASA kwa kushirikiana na RUWASA watakarabati miradi nane (8) pembezoni mwa mji katika maeneo ya Unyamikumbi A, Mtamaa B,  Manga, Ititi, Uhamaka,Unyianga Mtamaa A na Mwankoko A ambayo kwa sasa haitoi huduma  ya maji.

Ameendelea kusema kwamba wameweka mkakati wa kuhakikisha wanaongeza mtandao wa maji kwa kusambaza mabomba yenye urefu wa zaidi ya Kilometa 10 katika maeno ambayo hayana huduma hiyo.

Hata hivyo ameongeza kwamba changamoto kubwa katika utoaji wa huduma ya maji ni uhaba wa mitandao ya majitaka ambayo huathiri mazingira na tayari mipango ya uanzishwaji wa mradi huo umekamilika.

Changamoto chingine ni kupungua kwa uwezo wa visima kuzalisha maji na vingine kuwa na maji chumvi pamoja na uwepo wa mtandao wa mabomba ya zamani wenye urefu wa kilometa 40 ambayo husababisha upotevu wa maji. Alisema Mhandisi Patrick.

Aidha Mhandisi Patrick amemueleza RC kwamba baadhi ya wateja wamekuwa kikwazo kwa kuwa hawalipi madeni yao kulingana na huduma ya maji wanayoipata hivyo kusababisha deni la shilingi milioni 581.32 ambapo taasisi za Serikali pekee zinadaiwa kiasi cha shilingi milioni 305.
Share To:

Post A Comment: