Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph Kitukulu, akiwaonesha moja ya mashine zinazonunuliwa na MSD baadhi ya madaktari na Wataalam wa Maabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Mloganzila wakati akiwatambulishwa mashine na vitendanishi vya maabara vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa matumizi ya vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali nchini.

Utambulisho wa vifaa hivyo ukiendelea. Vifaa hivyo vinapima hematolojia(full blood picture), kemia ya mwili(body chemistry), wingi wa damu(hemoglobin), sukari(glucose), mkojo(urinalysis) na vichocheo vya mwili(hormones)
Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema Mwale, akizungumza na wataalamu hao kuhusu 
hatua ya MSD kununua vifaa hivyo kutoka kwa wazalishaji  na jinsi inavyochangia juhudi za serikali kuboresha huduma za afya za wananchi, na kuipunguzia serikali gharama kwa asilimia 40 hadi 50

 

Na Mwandishi Wetu.

BAADHI ya madaktari na Wataalam wa Maabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Mloganzila wametambulishwa mashine na vitendanishi vya maabara vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa matumizi ya vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali nchini.

Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph Kitukulu amewaeleza kuwa, mbali na vifaa hivyo kutumia teknolojia ya kisasa,kupunguza muda na kuwa na gharama nafuu vinauwezo wa kuchukua sampuli nyingi zaidi.

Kwa upande wake,Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema Mwale amesema kuwa hatua ya MSD kununua vifaa hivyo kutoka kwa wazalishaji itachangia juhudi za serikali kuboresha huduma za afya za wananchi, na kuipunguzia serikali gharama kwa takribani asilimia 40 hadi 50
Share To:

Post A Comment: