Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi (wa pili kulia) akizungumza baada ya kuona uendelevu wa Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) leo Jumapili Julai 11,2021.
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola (kushoto) akimwelezea Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi kuhusu Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga unaotekelezwa na SHUWASA kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akielezea jambo wakati Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akiangalia uendelevu wa Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakifungua maji katika Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, Koplo Rehema Haji akimtwisha ndoo ya maji Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) baada ya Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi kuangalia na kuridhishwa na uendelevu wa Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akifurahia akiwa amejitwisha ndoo ya maji baada ya Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi kujionea na kuridhishwa na uendelevu wa Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni mmoja wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, Koplo Rehema Haji
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 ukiwa katika Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi (wa pili kulia) akiangalia sehemu ya bomba la maji katika moja ya kaya ya mwananchi anayeendelea na ujenzi wa nyumba akitumia maji ya Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi (katikati) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola (kulia) akiangalia uendelevu wa Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mradi wa Maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga baada ya Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi kuona uendelevu huo wa mradi wa maji.
Muonekano wa sehemu ya mradi wa maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mradi wa maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mradi wa maji katika mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga.
 
 
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi ameridhishwa na uendelevu wa Mradi wa Maji Masekelo unaohudumia mitaa ya Masekelo, Ndala na kitongoji cha Ishoshandili katika Manispaa ya Shinyanga unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).

Akizungumza baada ya kuona uendelevu wa mradi huo wa maji leo Jumapili Julai 11,2021 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Paul Mwambashi amesema mradi huo utasaidia kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji karibu na kuwapunguzia adha ya maji wananchi.

“Tumekuja hapa kuangalia uendelevu wa mradi wa maji ambao ambao jiwe lake la Msingi liliwekwa Julai 11,2019 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali. Tumeona uendelevu sasa wananchi wameweza kuunganishiwa maji katika kaya zao na hii ni hatua kubwa kwa sababu maji ni uhai na itasaidia kupunguza adha ya wananchi kufuata maji mbali na kutumia muda huo kufanya shughuli za uzalishaji mali”,amesema Luteni Josephine Mwambashi.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru amelishukuru Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa kufadhili mradi huo wa maji huku akiwataka wananchi kutunza mradi huo.

“Niwasihi wananchi kuendelea kutunza miundo mbinu ya maji ambayo inatupatia huduma hii muhimu ya maji ili yatumiwe na vizazi vijavyo.Ni matumaini yangu wananchi watatumia fursa hii kutumia maji safi na salama na kutunza mabomba ya maji”,ameongeza Luteni Josephine Mwambashi.

Akitoa taarifa kuhusu Mradi wa Maji Masekelo, Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola amesema mradi huo umejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa kushirikiana na SHUWASA kwa gharama za shilingi 218,962,500/= ambazo zote zimetolewa na mfadhili huyo.

Amesema ujenzi wa mradi huo ulikamilika Mwezi Desemba 2020 ukihusisha ujenzi wa mtandao wa maji wenye urefu wa mita 11,225 na vituo 14 vya kuchotea maji (DP) na ufungaji wa dira 14 za malipo ya kabla.

“Ujenzi wa Mradi huu umezingatia mahitaji maalumu ya watu wenye mahitaji maalum kwa kujenga magati katika sehemu zinazofikika kwa urahisi. Mradi pia umeweza kuunganisha wateja wapya 230 hivyo kupelekea wakazi takribani 1,380 kupata huduma ya maji moja kwa moja kwenye makazi yao”,amesema.

“Lengo la mradi huu wa maji ni kuwapunguzia adha ya maji wananchi, kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji safi maeneo ambayo yalikuwa hayajafikiwa na Mtandao wa maji ya Ziwa Victoria”,ameeleza Mhandisi Katopola.

Aidha, amesema SHUWASA itaendelea kuhakikisha mradi huo wa maji unakuwa endelevu kwa kuhakikisha mradi unatoa maji safi na salama kwa muda wa saa 24 kila siku isipokuwa wanapokuwa na matengenezo.

“SHUWASA inaendelea kuwasihi na itaendelea kuwashawishi wakazi wa maeneo ya Masekelo, Ndala na Ishoshandili kutumia maji safi na salama na hasa kwa kujiunga kwenye mtandao wa mabomba ili kila mwananchi aweze kupata maji katika mji wake”,ameongeza Mhandisi Katopola.
 
Share To:

Post A Comment: