Meneja
wa Mradi wa Mkuju Bwa. Beria Vorster akionyesha kifaa cha kupimia
mionzi inayotoka katika madini ya ureniam kwa Bodi ya Wakurugenzi wa
NEMC.
Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Muhandisi Dkt. Samuel Gwamaka, akielezea jambo wakati wa ukaguzi wa
mradi wa Uraniam uliopo Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Bodi
ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), wakisikiliza maelezo yanayotolewa na Meneja wa Mradi wa uraniam
wa Mkuju kutoka kampuni ya Mantra Tanzania Limited Bwa. Beria Vorster.
Na Mwandishi wetu
BODIya
Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira
(NEMC), imefanya ziara katika mradi wa kuchimba madini aina ya uraniam
unaoendeshwa na kampuni ya Mantra Tanzania Limited, ambao unatarajia
kuanza kuchimba hivi karibuni madini hayo yatatumika kwa ajili ya
kuzalisha nishati ya umeme. Mradi uliopo maeneo ya Mkuju Wilaya ya
Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Bodi
hio imetembelea mradi huo ili kukagua na kujiridhisha kuhusu hali ya
kimazingira ili mradi utakapoanza usiwe na athari kimazingira na
kijamii bali uwe chachu ya maendeleo katika Taifa letu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Muhandisi Dkt.Samuel Gwamaka amesema kuwa, watu wengi katika jamii yetu
wamekuwa na uelewa mdogo juu ya madini haya aina ya uraniam kwani
wanaamini kuwa ni madini ambayo yanaathari kubwa katika mazingira na
afya za binadamu.
"Tutambue
kuwa kila Mradi unapotaka kuanzishwa katika Taifa letu unalazimika
kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na mradi huu umefanyiwa toka
2012. Sisi kama Taasisi tumejiridhisha kuwa athari zake ni ndogo.
Kimsingi mradi huu ulipewa kibali au cheti cha Tathmini ya Athari kwa
Mazingira toka 2012 ambapo pia walikuwa hawajaanza kuchimba mpaka sasa
hivyo pia tumekuja kujiridhisha kuhusu yaliyofanyika toka wapewe kibali
hicho."Dkt.Gwamaka
Kwa
upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Dkt. Catherine Masao
amesema kuwa, kama mradi huu utazingatia taratibu walizoeleza na
walizopewa na Baraza basi hautakuwa na athari ya kimazingira na kijamii.
"Mtazamo
juu ya madini haya ya uraniam kwa wananchi bado ni mbaya hivyo kuna
haja ya kutoa elimu kwa jamii ili kuelewa kwa undani wake. Mimi nikiwa
kama mwakilishi wa kimazingira nimebaini athari zitokanazo na uraniam ni
kutokana na kula na kuvuta kwa muda mrefu hivyo tutoe elimu kwa jamii
watambue hili." Dkt. Catherine
Naye
Fredrick Kibodya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania
Limited amesema kuwa, Mradi unafaida kubwa kwa jamii na kitaifa endapo
utaanza utasaidia kutoa ajira kwa vijana kwani wanatarajia kuajiri watu
wengi sana pamoja na hayo mradi utachangia mapato makubwa ya Taifa.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi na mradi kwa upande wa
kimazingira na kiafya wamejipanga katika kudhibiti athari zote
zitokanazo na uchimbaji wa uraniam, pia amesema kuwa kutokana na mradi
huo kuwepo ndani ya Hifadhi watahakikisha miti na wanyama wanabaki
salama.
Kwa
upande wake Afisa muandamizi wa NEMC Muhandisi Dkt. Befrina Igulu
amesema kuwa, NEMC ni Taasisi inayohusu mazingira itambulike kuwa
uchimbaji wa madini ya uraniam unafanyika ndani ya Hifadhi hivyo unaweza
kuathiri mazingira kwa namna moja ama nyingine, hivyo NEMC imekuja
kuangalia namna gani utekelezaji wa mradi huo hauta athiri Mazingira.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasiwe na hofu juu ya utekelezwaji wa mradi huo,
kwani serikali itasimamia na kuhakikisha maisha yao na viumbe hai
vingine vinakuwa salama.
Post A Comment: