Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Ndg, Emmanuel Tutuba akiongea na Wahariri wa vyombo Mbali mbali vya Habari hapa Nchini katika ukumbi wa Hazina Ndogo Jijini Arusha.

        Na Lucas Myovela_ Arusha.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Ndg.Emmanuel Tutuba amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kutoa elimu na upatikanaji wa habari zenye usahihi kwa jamii kuhusu utekelezaji wa Programu ya PPP nchini ili kusaidia jitihada za upatikanaji wa maendeleo ya nchini.

Akifungua mafunzo ya PPP kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika jijini Arusha Ndg.Tutuba amesema programu ya PPP nchini ina umuhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Tutuba amezitaka mamlaka za serikali zilizopewa jukumu la kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta zinazosimamia kutumia ipasavyo utaratibu wa PPP kwa miradi yenye sifa za kuihusisha sekta binafsi katika kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo yenye uwezekano wa kuishirikisha sekta binafsi badala ya kutegemea bajeti ya serikali.

"Serikali imeweka taratibu hizi ili kufanikisha kufikia malengo ya mipango ya maendeleo ya nchi ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025,mpango wa tatu wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano pamoja na ilani ya chama cha mapinduzi."Tutuba

Ameongeza kuwa pamoja na changamoto za ushirikishwaji wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,serikali kupitia wizara ya fedha na mipango inahakikisha miradi iliyopangwa kutekelezwa katika Programu ya PPP inafanyiwa uchambuzi wa timu za wataalamu zinazoundwa kutoka katika taasisi mbalombali za serikali.

Vilevile ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa Programu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi ambapo Serikali imeandaa Programu ya PPP nchini ili kuwezesha sekta binafsi kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Naye mwenyekiti wa mafunzo Ben Mwang'ombe ameishukuru wizara hiyo kwa kuandaa mafunzo ambayo yatawasaidia wahariri wa vyombo vya habari kutoa sera za kiuchumi kwa jamii.

“Serikali imetunga Sera ya PPP ya Mwaka 2009, Sheria ya PPP Sura 103 na Kanuni za PPP za Mwaka 2020 ili kuweka mazingira wezeshi ya kuishirikisha Sekta Binafsi kwa utaratibu huo wa PPP”, alisisitiza Dkt. Mboya.
Share To:

Post A Comment: