Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kufika kwenye banda la Wizara tarehe 03.06.2021 na kujionea
shughuli zinazofanywa na Sekta ya Mifugo na Uvuvi Katika utunzaji na
uhifadhi wa Mazingira kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
inayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma
Nahodha
Mwandamizi kutoka Idara ya Uvuvi Bw. Dickson Stowa akitoa maelezo kwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki juu ya Uhifadhi na
Usimamizi wa Mazingira kwa kutumia Zana za Uvuvi tarehe 03.06.2021
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika
Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki akipatiwa maelezo ya namna ya
kuandaa udongo wa kuoteshea miche kwa ajili ya kutunza Mazingira na
Mkurugenzi Mkuu wa mradi wa "The Young World Feeders" Bw. Ray Peter
alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo tarehe 03.06.2021 kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika Viwanja vya
Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba
Ndaki amesisisitiza wananchi kutumia nishati mbadala ili kuhifadhi na
kutunza mazingira kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi
Waziri
Ndaki ameyasema hayo leo tarehe 03.06.2021 alipotembelea baadhi ya
mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira inayofanyika Katika
Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Centre ,Jijini Dodoma na kusisitiza
elimu zaid juu ya nishati mbadala Kwa Wananchi ili kutunza
Mazingira vizuri.
“Tujali
sana kutunza mazingira tunapofanya shughuli za kiuchumi na kijamii,
kwenye shughuli za kufuga na kuvua lazima tujali kuhifadhi mazingira,
tusipohifadhi mazingira tutakosa na mazalia ya samaki na samaki watakosa
chakula”,amesema Waziri Ndaki.
Mhe.
Ndaki amesema kuwa ili shughuli zetu za ufugaji na uvuvi ziweze
kuendelea tuhifadhi kwenye maeneo ya nchi kavu, bahari , mito, maziwa na
maeneo ya misitu ili ziweze kuwa endelevu.
“Watanzania
tutunze mazingira ya nchi yetu ili yaweze kututunza”alimalizia Waziri
Ndaki alipokuwa akihitimisha wito wake kwa Wananchi .
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani (Sekta ya Mifugo) Dkt.
Kejeri Gillah amesema kuwa, wafugaji wazingatie namna bora ya kufuga
mifugo yao, kuhifadhi na kutunza mazingira vizuri.
“Kabla
ya kupanda malisho ni vizuri kujua mbegu inayostahimili ikolojia na
wafugaji wazingatie malisho yanayostahimili katika maeneo husika”,
alisema Dkt. Gillah.
Aidha,
Dkt. Gilla amebainisha kuwa watu wanapochinja Mifugo yao takataka
zinazotokana na Mifugo hiyo inaenda kuchafua mazingira, hivyo tunashauri
wafugaji kuzingatia namna bora ya kutunza Mifugo na mazingira.
Naye,
Mkuu wa kitengo cha mazingira (Sekta ya uvuvi) Bw. Melton Kalinga,
amesema kuwa lengo la maonesho haya ni kutumia zana za uvuvi rafiki kwa
mazingira kwa ajili ya kutunza viumbe hai majini, hususani samaki.
Aidha,
Nahodha Mwandamizi kutoka Idara ya Uvuvi Dickson Stoah ameongeza kuwa,
uharibifu wa mazingira unatokana na Utumiaji wa zana haramu majini na
hivyo kuathiri mfumo mzima wa viumbe maji.
Kwa
upande wa Wadau wa mazingira waliokuwa wanatembelea mabanda, baadhi ya
washiriki wameipongeza Serikali kwa kuweka Maadhimisho hayo kwa ajili ya
kuelimisha na kujifunza juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa
kutumia nishati mbadala kuongoa mfumo wa ikolojia.
Maadhimisho
ya siku ya mazingira Duniani yatahitimishwa tarehe 05.06.2021 Jijini
Dodoma Katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Centre ambapo kauli
Mbiu yake ikiwa inasema “Tutumie Nishati Mbadala kuongoa mfumo wa
Ikolojia”.
Post A Comment: