Leo Juni 4, 2021 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu tuhuma zinazowakabili.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na wenzake.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi ya Mei 13, 2021 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa, Sabaya alisimamishwa kazi kuanzia tarehe hiyo.

Rais Samia alichukua uamuzi huo ikiwa mheshimiwa Sabaya amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka michache tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli Julai 28, 2018.

Chanzo - Dira Makini
Share To:

msumbanews

Post A Comment: