Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma


Watanzania wametakiwa kuja na mtazamo chanya kuwa kilimo ni sehemu  ya kazi muhimu na nyeti na kuondoa mtazamo hasi na potofu kuwa kilimo ni  kazi ya watu masikini.


Hayo yamebainishwa Juni 17,2021  Jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Omary Mgumba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa  11 wa wadau wa zao la kahawa  kwa Mwaka 2021  ambapo amesema wakati mwingine baadhi ya walimu wamekuwa wakichangia kudumaza kilimo na kuona kuwa kilimo ni sehemu ya kumwadhibu mwanafunzi bali ni stadi za mafunzo kama zilivyo kazi zingine .


"Hatuwezi piga hatua kama kwenye suala la kilimo tunafanya blaablaa na kufikiri kuwa mtu anayelima ni masikini na hana mwelekeo,mawazo haya tuyaondoe ,unakuta mwalimu anamwazimu mtoto kwenda kulima shamba hii ni dhana mbovu inayojengeka kuwa kilimo sio kazi nyeti na ni kazi ya watu masikini tubadilike" amesema.


Hivyo Mgumba amesisitiza kuwa  ni vyema walimu wakatambua kuwa kilimo ni moja ya stadi muhimu huku akitoa akibainisha kuwa ni Serikali imeendelea kuweka kipaumbele mazao ya kimkakati ikiwemo zao la kahawa licha ya kukumbwa na changamoto kutokana na wakulima kutojikita zaidi kwenye zao hilo licha ya kuwa na soko.


 Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania Profesa Aurelia Kamuzora amesema ni vyema kila mkulima kujikita katika kilimo chenye tija.


"Tunaposema tija ni kulima shamba dogo mavuno mengi,hivyo ni muhimu kila mkulima akawekeza kulima kwa tija na si kuwa na shamba kubwa mavuno kidogo " amesema.
.


Nao baadhi ya Wadau   wa zao la kimkakati la kahawa  akiwemo Jensen Fredick  pamoja na Mary Mgitu wamesema  kuwa mkutano huo utawawezesha  kulima kwa tija ili kuwendana  na mahitaji ya soko ndani na nje ya nchi.


Aidha, wamesema ardhi Tanzania inaendelea kupungua kutokana na kuongezeka idadi ya watu huku wakizungumzia umuhimu wa suala la ubora wa mbegu ili kupata masoko mazuri zaidi.


Hata hivyo wadau hao wamesema bado kuna changamoto ya upungufu wa maafisa ugani katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa kahawa .


Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa umeanza Juni 17-18,2021 ukienda sambamba na kaulimbiu isemayo"Uzalishaji wenye tija,ndio nguzo ya maendeleo ya sekta ya Kahawa.


MWISHO

Share To:

msumbanews

Post A Comment: