Kaimu Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani  (kulia) akiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Aloyce Gonzaga-Minga Singida,  Padri Festo King'wai baada ya kutembelea parokia hiyo na kuzungumza na  baadhi ya vijana.wa Parokia hiyo,.

Vijana wakiwa katika Parokia hiyo.

Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.




Na Dotto Mwaibale, Singida



KAIMU Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewashauri viongozi wa dini mkoani hapa kuwasaidia vijana kijikwamua na umaskini kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi katika maeneo wanayoishi na ndani ya madhehebu yao ya dini .

Makanisa na misikiti ina maeneo makubwa ambayo yakiratibiwa vyema na kupewa vijana itawasaidia na kuwasaidia viongozi wa dini katika maeneo yao.

Ndahani aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Vijana wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minga  mkoani hapa.

" Vijana walio katika mathehebu ya dini wanayo sifa ya kupata mikopo ya elimu ya juu ya kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na shughuli zingine za kiuchumi." alisema Ndahani.

Ndahani aliwaombe viongozi wa dini kuwahamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii huku wakimtumikia Mungu ili kujiletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya vijana hao, Happiness Kilawe  alisema wamepokea kwa mikono miwili ushauri waliopatiwa na Ndahani na kuwa wataufanyia kazi.

"Katika eneo la kanisa kuna zaidi ya ekari nane ambazo zipo  tu bila kufanyiwa shughuli yoyote ambapo tukipatiwa tunaweza kuanzisha miradi kama ya ufugaji na kilimo na kujipatia kipato." alisema Kilawe.
Share To:

Post A Comment: