Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizundua upatikanaji wa umeme katika kijiji cha Holo kilichopo wilaya ya Ismain mkoani Iringa

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato akiongea na wananchi wa kijiji cha Holo wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC)

Baadhi ya wanakamati wa kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kijiji cha Holo wakati wa ziara ya kamati hiyo.

 
Na Fredy Mgunda.Iringa.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utendaji kazi wa wizara ya nishati katika swala zima la kuwapelekea wananchi umeme vijijini kwa gharama nafuu kupitia mradi wa REA na kutoa maagizo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na wizara hiyo.

Akizungumza mara baada ya ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa kwa kiasi kikubwa wizara ya nishati imefanya kazi kubwa ya kupeleka umeme vijijini na kuwaongezea kasi ya kufanya shughuli za kimaendeleo.

Alisema kuwa wamefanikiwa kutembelea kijiji cha Holo kilichopo katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na kubaini kuwa kwa asilimia kubwa wananchi wamepatiwa umeme licha ya baadhi ya vitongoji na kaya bado hawajapata umeme jambo ambalo linaweza kushughulikiwa na wizara kwa sababu lipo katika uwezo wao.

Licha ya kazi nzuri inayofanywa na wizara hiyo kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeiaigiza wizara ya Nishati kuhakikisha inawasimia watendaji wa Tanesco ili waweze kuwahudumia wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo kwa ajili ya maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Kaboyoka alisema kuwa wakandarasi wengi wamekuwa wanafanya kazi kinyume na mikataba yao hivyo ni lazima wizara kuhakikisha inawasimamia vilivyo ili kuhakikisha fedha za serikali hazipotei bila sababu ya msingi.

Aliitaka wizara ya nishati kuhakikisha inasimamia vilivyo mapato ya wananchi kwa kuhakikisha kila kazi inayofanywa  na watendaji  na wakarasi inaendana na gharama za kazi iliyofanywa na sio vinginevyo.

Lakini pia kamati ililitaka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linafanya kazi kwa weredi unaotakiwa ili kuondoa makandokando ambayo yamekuwa yanajitokeza mara kwa mara katika shirika hilo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na kamati wakati wa ziara na watayafanyia kazi na maagizo mengine tayari yameshafanyiwa kazi.

Naibu Waziri Byabato alisema kuwa serikali imetumia zaidi ya bilioni 30 kupeleka umeme wa REA katika vijiji na vitongoji vya wa mkoa wa Iringa ambapo hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili mwaka 2022 vijiji na vitongoji vyote vitakuwa vimepata umeme wa REA.

Naibu Waziri Byabato alisema kuwa katika mkoa wa Iringa wenye vijiji 354 kwa asilimia kubwa vijiji vimepata umeme ilisipokuwa vijiji 31 ndio bado havijapata umeme na vinatarajiwa kupata umeme kabla ya mwezi  wa kumi na mbili mwaka 2022.

Alisema kuwa taasisi zote za serikali na ambazo sio za kiserikali kwa lengo la kukuza uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi ambao wanafikiwa na nishati hiyo.

Aidha naibu waziri Byabato alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanailinda miundombinu yote inayotumiwa na shirika la umeme Tanzania kwa lengo la kuepuka kutumia vibaya pesa za wananchi na kuwaomba wananchi nao kuilinda miundombinu hiyo.

Naibu waziri Byabato alimalizia kwa kuimbia kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa wizara imeamua itawalipa wakandarasi kutokana na kazi iliyokamilika na hawatatumia tena mfumo wa awali waliokuwa wanautumia.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Holo Wiston Mpalazi alisema kuwa licha ya kufisha umeme katika kijiji hicho bado kuna baadhi ya vitongoji na kaya hazijafikishwa huduma ya nishati ya umeme wa REA hali inayoendelea kuzua maswali kwa wananchi.

Licha changamoto ya baadhi ya vitongoji kutofikiwa na umeme waliipongeza wizara kwa kazi waliyoifanya kuifikisha umeme katika kijiji hicho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: