Na Woinde Shizza , ARUSHA


Kutokana na tatizo la kutokuwepo kwa ajira nyingi  za moja kwa moja za serikalini , wanafunzi wa vyuo vikuu wametakiwa kujiongeza na kuwa na kitu cha ziada  Cha kufanya nje na taaluma ambazo wanazo ili waweze kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao.


Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa Phid Intertaiment &tours  ambaye pia ni muandaaji wa Tuzo za wanawake na wanaume  zijulikanazo kwa jina la Extraordinary men awards 2021 pamoja Mwanamke Tuzo 2021 ,Phidencia Mwakitalima alipokuwa akiongea katika uzinduzi rasmi wa Tuzo hizo za wanaume pamoja na ugawaji wa zawadi ya Tuzo ya mwanamke uliofanyika jijini hapa.


Alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la ajira za serikalini na hata binafsi,wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma lakini baada ya kumaliza wanaenda kukaa tu mtaani bila ya kazi yeyote na hii inatoka na kukosa ajira na ujuzi wa vitendo.


Aliwataka wanaume na wanawake kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa huku wakiamini kwamba kuna watu wengine huko nje wanatambua mchango wao.


Alisema kuwa tuzo hizi zitasaidia kuwapa motisha wanawake wajasiriamali ,wanaume pamoja na wanafunzi  kufanya kazi kwa  bidii ,kwani inawasaidia pia kujitangaza  ,pamoja na kuwa wamoja pamoja na kuwakutanisha  na watu mbalimbali,kujifunza mambo mbalimbali haswa katika biashara zao bila kuangalia matatizo ambayo wanakabiliana nayo.


"Tuzo hizi tumezigawa Katika makundi mbalimbali tukianza na tuzo ya mwanamke bora mjasiriamali,wanawake bora wa kikundi wajasiamali pamoja na binti mjasiriamali na kwa wanaume Kuna tuzo za kiongozi bora , mwanafunzi bora mjasiriamali,pamoja na kiongozi  bora"alisema Phide


Kwa upande  wake afisa utamaduni wa jiji la Arusha Elizabeth Ncheye alipongeza kampuni hii ya Phide Intertaiment  kwa kuandaa tuzo hizi ambapo alizitaka kampuni zingine za sana ziendelee kuiga mfano huu wa kuandaa tuzo mbalimbali kwani zinasaidia kutoa hamasa kwa jamii yetu na kuwatia moyo wanajamii ambao wanajihisisha na shughuli nzima za ujasiriamali ambapo alifafanua wakizungumzia ujasiriamali ndani yake kuna ubunifu  ndani yake kinapatikana kitu kinaitwa sanaa na ndio maana baraza la sanaa linasimamia zoezi la tuzo 


Aliwataka wanawake wengi  ,wanafunzi na wanaume waweze kushiriki kwa wingi katika Tuzo hizi kwani zinasaidia Sana kuwatangaza  na kukuza biashara zao zaidi


Kwa upande mmoja wapo wawashindi wa Tuzo za wanawake ambaye pia ni mmiliki wa maduka ya nguo yajulikanayo kwa jina la new look braido  , Elizabeth Mayani (mama shombee)alisema tuzo hizi zimeweza kumsaidia kukuza biashara yake kwani tangu ameweza kupata tuzo hii amepata kazi nyingi ikiwepo ya kumvalisha mtoto wa Mchungaji mkubwa duniani ajulikanae kwa jina TB Joshua ,ambapo alimvalisha mtoto wake wa kike ajulikanae kwa jina la  Serah Katika harusi yake uliofanyika mkoani hapa.

Aliwataka wanaume na wanawake kushiriki tuzo hizi kwani zinasaidia kukuza biashara zao kwa haraka na zinawafanya wajulikane zaidi.

Tuzo hizo za wanawake zinafanyika kila mwezi tatu ya kila mwaka na kwa upande wa Tuzo za wanaume zitafanyika kila mwezi July 20 ya kila mwaka .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: