Jane Edward, MsumbaNews, Àrusha


Waziri wa fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za fedha zenye sifa za kutoka nje ya nchi kufungua matawi katika nchi hizo ili kukuza uchumi pamoja na kuongeza ajira, ambapo ameielekeza Benki Kuu ya Tanzania kufanya utafiti wa ufunguaji wa matawi ya kibenki katika nje ya nchi.Akifungua semina ya wanahisa wa benki ya CRDB Dkt.Mwigulu Nchemba ameitaka Benki hiyo kutoa elimu ya kifedha kwa wanahisa na watanzania kwa ujumla kwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla maana mwanchi akijua elimu ya fedha ni rahisi kuwa na utumiaji wa fedha kwa ufanisi.


Aidha alisema kuwa kuimarika kwa utendaji wa Benki hiyo kunatokana na uboreshwaji wa mfumo wa utendaji na uwekezaji katika mifumo ya kidigitali jambo ambalo limesaidia kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wateja na kuifanya benki ya CRDB kuendelea kutengeneza faida na kutoa gawio kwa wanahisa wake.


Dkt.Mwigulu ameahidi sera nzuri za kifedha na ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kifedha na kujenga mazingira wezeshi ili sekta ya fedha na benki ya CRDB waweze kufanikiwa zaidi ikiwa ni pamoja na kupunguza riba iliyopo kwenye mikopo.


Kwa upande wake Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt.Bernard Kibese kutokana na semina hiyo kujielekeza katika kuongeza ufahamu katika masuala ya elimu ya fedha na uwekezaji jambo ambalo ni muhimu kwa ustawi wa sekta ya fedha ambapo ameziagiza taasisi za fedha kupunguza riba wanazotoza wananchi wanaowapatia mikopo kwa kuwa riba hizo zinawaumiza wananchi.


Naye Mwenyekiti wa bodi ya CRDB  Dky.Ally Laay amesema kuwa wastani wa hisa milioni moja na laki 7 hununuliwa kwa wastani wa shilingi milioni mia nne siti ambapo takwimu zinaonyesha watanzania wasiozidi laki 7 kati ya watanzania milioni ambao wamewekeza kwenye hisa na makampuni mbalimbali sawa na asilimia 1.25 ukilinganisha na wastani wa hisa milioni kumi na tisa zinazonunuliwa na kuuzwa katika soko la hisa la Nairobi kwa zaidi ya shilingi bilioni 10 ukilinganisha na mnada wa soko wa hisa za Dar es salaam na Nairobi upo tofauti.


Ameongeza kuwa kazi kubwa ipo ya kuhamasisha wateja kuwekeza kwenye hisa kwa ufahamu mdogo uliopo juu ya masuala ya hisa na uwekezaji kwenye soko la hisa,ambapo amesema pamoja na juhudi zinazofanyika bado taifa la Tanzania lipo nyuma.


Ameeleza kuwa ipo haja ya kuongeza elimu kuhusu uwekezaki katika soko ili vijana waweze kupata ufahamu wakiwa bado wadogo hali itakayobadilisha mtazamo kusudi kuweza kuleta fikra chanya kwenye uwekezaji hivyo jambo hilo Dkt.Laay ameomba kwenye mitaala ya wanafunzi itazamwe somo la hisa ili waweze kufahamu wakiwa bado wadogo.


Sambamba na hayo Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dkt.Charles Kimei katika semina hiyo alisema kuwa kutokana na faida za benki hiyo kupanda kutokana na njia mbadala iliyoitumika katika kutoa huduma kwa njia ya kidigitali ambapo ameiomba benki hiyo iwapunguzie riba za mikopo ambazo zipo juu kwa asilimia 15 ili kuweza kuwawezesha wakopaji wateja kufaidj kwa kuweza kuchukuwa mikopo ambayo itakuwa na riba nafuu pamoja kufikiria kuongeza riba ya waweka amana.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: