Na Woinde Shizza, 


Uongozi  shule za  BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA  pamoja na BLESSINGS DAY umempongeza Rais wa Jamuhuri ya  muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama  Samia Suluhu kwa kuanza vizuri  kazi yake na kukubalika na makundi yote katika jamii ya watanzania.


Pongezi hizo zimetolewa na muwekezaji  wa shule hizo ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Mwl.Ezekiel Eliphas  Meivule Mollel ambapo  alimuahidi  Rais Samia kumpa  ushirikiano  wa asilimia zote katika sekta ya elimu.


Aidha pia alisema kasi aliyoingia nayo Rais Samia ni nzuri na anauhakika kabisa itaweza kuivusha nchi ya Tanzania , na kuwafikisha watanzania mbali zaidi katika swala la Maendeleo ukizingatia nchi yetu ina vitega uchumi vingi.


 Aliongeza kuwa wataendelea kumuweka katika  maombi yeye na viongozi wenzake wa serikali ili waweze  kuyatekeleza yale yote ambayo amekusudia kuwafanyia watanzania ikiwemo kumaliza miradi yote mikubwa iliyoachwa na hayati John  Magufuli  pamoja na kuwaletea maendeleo   ya nchi pamoja na mtu mmoja mmoja.


 Alisema wanaona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi pamoja na kusaidia   katika kuleta Maendeleo ya nchi .


Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuongeza ajira kwa walimu 6000 ambao wapo mtaani na kusema kuwa hii itadaidia kuboresha elimu yetu iendelee kuwa bora zaidi,pia alipongeza mikakati mipya aliyoitagaza ikiwemo kuhamasisha  uchimbaji wa madini 


Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano  wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi  hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza  wakafanya  mambo yakaenda sawa.
Alibainisha kuwa jamii yenye ufahamu wa kutosha juu ya wajibu wake katika utawala bora, demokrasia na haki za binadamu, ni jamii inayowajibika na inayoshiriki 

kikamilifu, na kwa hiari katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa taifa.


Mwisho.Picha  mwekezaji wa  shule za BLESSINGS MODEL SCHOOL MWANZA NYASAKA  pamoja na BLESSINGS DAY

Hide quoted text

 zilizopo mwanza ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi  Ezekiel Mollel akiongea na michuzi Tv

Share To:

msumbanews

Post A Comment: