Na Woinde Shizza 

Mchimbaji mdogo  wa Madini ya Ruby yaliyopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido Mkoani Arusha Sendeu Laizer amempongeza Rais Samia Suluhu kubaini mwenendo usioridhisha wa ukusanyaji kodi pamoja na kuruhusu wachimbaji Madini kuendelea kuchimba Madini


Aliyasema hayo leo wakati akiongea na waandishii wa hatari ambapo  alisema kuwa baada ya kuwaapisha mawaziri Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia alimtaka Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kutanua wigo wa ukusanyaji kodi akionya kile alichokiita kuwaua walipa kodi kwa kufunga biashara zao, kuchukua fedha na vifaa vyao vya kazi pamoja na kufunga akaunti zao.


Alisema kuwa kauli hiyo imerejesha amani kwa wafanyabiashara na itaongeza uwekezaji chini Katika sekta mbalimbali ikiwemo ya madini


“Tunampongeza sana Rais na tunamuunga mkono ambacho kilikuwa kinafanyika ni kibaya sana, watu kuvamia katika biashara, kufunga akaunti na kuchukua fedha,  kwa nchi nyingine ni kesi kubwa tunamuombea mungu aendelee kumlinda," alisema.


Alisema kauli hii itasaidia sasa wafanyabiashara kuendeleza biashara zao na kulipa kodi ya Serikali lakini bila kuua biashara zao


 Sendeu Laizer ambaye kampuni yake hivi karibuni  ilipewa  tuzo na serikali ya upambanaji kwa jitiada kubwa alizofanya bila kukata tamaa ,ambapo alizingatia sheria zote za nchi pamoja na sheria zote za uchimbaji wa  madini  ,uhuzaji wa madini na uhusiano


Alisema tuzo hiyo  alikabidhiwa na Rais wa sasa wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia 

Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Samia Suluhu  kwa niaba ya hayati Rais magufuli kipindi alipokuwa makamu wa rais. 


 cha kutambua mchango wake sekta ya biashara ya madini ya vito, amesema  Rais ameonyesha huruma kwa wafanyabiashara na watahakikisha wanahamasishana kulipa kodi. 


Aidha alimpongeza Rais kwa kuweza kuhamasisha  uchimbaji wa madini , kwani utawezesha wawekezaji wengi wa ndani na nje kujitokeza kuja kuchimba Madini hayo.
Aliwapongeza watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kutunza amani na mshikamano wa nchi yetu ,ambapo aliwasisitiza watanzania kuendelea kumuenzi hayati Rais John Magufuli ambaye aliwaonyesha watanzania njia ya kuthubutu kwamba wanaweza wakafanya mambo yakaenda sawa.


Picha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akimkabidhi bilionea Sendeu Laizer tuzo wakati alipokuwa makamu wa rais.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: