Na Andrew Chale


KAMPUNI ya 361 Degrees ya Jijini Dar es Salaam imeandaa tuzo maalum za wauzaji na watoa huduma za Harusi ambazo zitakuwa zenye ufanisi na ubora  zitakazofahamika kama 'Harusi Awards' zinazotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena, Dar es Salaam, jioni ya Mei 16 mwaka huu.


Akizungumza wakati wa utambulisho rasmi wa tuzo hizo kwa Vyombo vya Habari, mapema leo, Waratibu wa tuzo hizo, kutoka 361 Degrees,  Benedict Msofe  alibainisha kuwa, wameanzisha Tuzo za Harusi  ili kutambua na kutunuku ufanisi na ubora kwenye sekta ya Harusi.


"Tunayo furaha kutangaza tuzo za kwanza katika sekta hii ya harusi hapa nchini, tuzo zenye ubora na ufanisi mkubwa.


Tayari tuna jumla ya washiriki  sitini na tano (65) watakaowania tuzo hizo katika vipengele  Ishirini (20)."  Alisema Benedict Msofe.


Benedict Msofe aliongeza kuwa, kuanzishwa kwa tuzo hizo ni kutokana na uzoefu wa muda mrefu walionao kwenye sekta ya Harusi kwa zaidi ya miaka nane (8).


"Tumekuwa kwenye uratibu wa sekta ya harusi kwa miaka Nane (8) sasa ikiwemo kuandaa maonesho ya harusi maarufu kama 'Harusi Trade Fair', kati ya mwaka 2010 hadi 2017 hivyo kuwa wabobezi kwenye sekta hii ya harusi".  Alisema Benedict Msofe.


Aidha, alisema washiriki wanatatajiwa kupatina kupitia kura zitakazopigwa kwa njia ya mtandao 'Online' huku zikisimamiwa na Washirika wakaguzi kampuni ya Innovex Tanzania.


"Ttukio la kupiga kura litaenda ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kupitia tovuto maalum. Ni jambo la kila mshirikia kuhamasisha watu ama wadau wao kuweza kuwapigia kura." Alimalizia Benedict Msofe.


Kwa upande wao washiriki upande wa kusimamia zoezi la kura, kutoka Innovex, Bi. Upendo Fatukubonye  alisema wao watahakikisha wanasimamia zoezi hilo na mshindi apatikane kwa haki.


"Lengo ni kuhakikisa haki inatendeka na tutaendesha kwa uhuru na haki". Alisema Bi. Upendo.


Kwa upande wake,  mwakilishi kutoka hoteli ya Serena, Seraphin Lusala alisema kuwa, wamejisikia furaja kuwa miongoni mwa wadhamini wa tuzo hizo kwani wao ni miongoni mwa wadau wakubwa wa sekta ya harusi.


"Hoteli ya Serena tunayofura kubwa kuwa miongoni mwa wadhamini kwani ni wadau wakubwa ikiwemo kutoa huduma za harusi kama kumbi za sherehe, eneo maalum la picha za kumbukumbu pamoja na eneo maalum la mapumziko baada ya ndoa (fungate)." Alisema Lusala.


Vipengele vya tuzo hizo vinavyowaniwa ni pamoja na: 


"Bridal hair & Make-up artist  of the year, Henna artis of the Year, Jewellery store of the year, Lfe time Archievement  of the Year, Pre-wedding mentor [somo] of the year.


Pia kuna:

"Wedding accessories store of the year, Wedding cake bakaer of the year, Wedding catere and desert maker of the year, Menswear designer of the year Wedding floriest of the year, Wedding gown designer and Boutique of the year.


Wedding MC of the year, Wedding transport provider of the  year, Weddig venue of the year, Wedding Salon/Spa ofe the year, Wedding set and decor of the year, Wedding Photographer of the year, Wedding stationey Supplier of the year na  Wedding Videographer of the year.


Tuzo hizo zinatarajiwa kuleta chachu kwa washiriki kujiongezea wateja  na ubora kwenye shughuli zao za kila siku kwenye sekta ya harusi.Share To:

msumbanews

Post A Comment: