Mfanyabiashara bidhaa kww njia ya mtandao Clamance Mtembela akizungumzia bei ya bando kuwa chini.

Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Hamisi Mchuchuri akizungumza faida ya kushuka kwa bando kurejea Awali kuwa kunapunguza gharama za maisha kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mjasirimali wa Biashara ya Matunda Walter Hiristo akizungumza kuhusiana watoa huduma kuboresha huduma ya bando na kuipongeza TCRA kwa udhibiti .

Mkurugenzi wa TIBA Marcela Lungu akizungumza faida ya kushuka kwa bando inavyotoa fursa katika uendeshaji wa Ofisi katika ununuzi wa vifurushi vya Internet.


*Wadai maisha yatakuwa rahisi katika kufanya biashara mtandaoni

Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kurudisha vifurushi vya Bando wananchi wamekuwa na maoni tofauti juu ya kuipongeza Mamlaka hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumiaji wa vifurushi vya Bando la Internet wamesema kuwa maisha yalikuwa magumu kwao na huku baadhi wakishindwa kuendesha biashara kwa kutumia mtandao.

Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji ( NIT) mwaka wa tatu Hamisi Mchuchuri amesema kuwa bando kuwa juu lilikuwa linawaathiri katika masomo kutokana maisha ya Chuo kuwa ya bajeti.

Amesema kuwa kuna vitabu vingine viko mtandaoni hivyo bila kuwa fedha zaidi ya 5000 huwezi kupata lakini sasa unapata hata sh.1000 na 2000 na kupata vifurushi vya kuweza kupakua vitabu vyote.

Mchuchuri amesema TCRA kupitia watoa huduma za simu wameweza kuboresha huduma za bando.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhamamasishaji wa Wanawake kutumia mitandao (TIBA) Marcela Lungu amesema kuwa kama wanaasasi walikuwa wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya bando lakini sasa itapungua na kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati.

Amesema wakati Ugonjwa wa Corona sehemu kubwa wanatumia mitandao kwa kununua bando kuendesha mikutano.

Kwa upannde wa Mjasirimali wa matunda Walter Hirispo amesema miasha ya bando kuwa juu yanaathiri watu wote hasa wenye kipato cha kuwaida kushindwa kumudu maisha hayo.

Nae Clemance Mtembela mfanyabiashara wa Duka Mtandao amesema kuwa biashara ya bando kurejea katika hali ya awali kumerahisha maisha kwa kuweza kuwafikia wateja wote kwa wakati na wakawa hewani.

Amesema wakati vifurushi vilivyokuwa juu baadhi ya watu walikuwa hawaingii mtandaoni kufanya biashara na hata wakiingia hawawezi kupakua huduma ndani ya mtandao


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: