Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,amesema kuwa amewaweka kikaangoni wakurugenzi wa halmashauri nane ambazo zimepata hati chafu kwa ajili ya kutolea maamuzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Habari leo Machi 28,2021 Jijini Dodoma,Mhe.Jafo amesema kuwa atawasilisha majina ya Wakurugenzi hao kwenye Mamlaka yao Uteuzi kwa ajili ya hatua stahiki.

“Kwakuwa Wakurugenzi wa Halmashauri Mamlaka yao ya Uteuzi ni Rais, nitawasilisha majina yao ili wachukuliwe hatua kwa kadiri atakavyoona inafaa,”amesema Jafo.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ­CAG iliyowasilishwa leo kwa Rais Samia Ikulu Chamwino imebainisha kuwa katika ukaguzi katika mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri nane zimepata hati chafu.

Mhe.Jafo amesema kuwa  licha ya kutoa mafunzo  na maeleekezo mbalimbali ya udhibiti na usimamizi wa fedha lakini halmshauri zao zimefanya vibaya, hivyo Ofisi ya Rais-TAMISEMI imejipanga kuchukua hatua kali kwa halmashauri hizo nane.

Aidha Mhe.Jafo amemuagiza Katibu Mkuu kuanza kufanya uchambuzi wa taarifa ya CAG, kisha kuwaondoa katika nafasi zao wawekahazina na wakaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo.

Hata hivyo Mhe. Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala ambao halmashauri nane zilizopata hati chafu kujitathimini kwa sababu viongozi hao walipaswa kushauri mwenendo wa matumizi ya fedha za serikali katika halmashauri zao.

Wakati huo huo,Waziri Jafo amewataka watendaji wote katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu kwa lengo la kuwatumikia wananchi.

Share To:

Post A Comment: