Na Woinde Shizza , ARUSHA

 Mkuu wa Wilaya ya Karatu Abbas Kayanda  amesema kuwa  hataki ufaulu wa daraja sifuri katika mtihani ya kitaifa wa kidato cha nne na mitihani wa kidato cha pili , nakubainisha kuwa ufaulu wa mwanafunzi unaanza kwa mwanafunzi kupata ufaulu wa  alama D mbili nani jambo linalowezekana kufanyika.

Aliyasema hayo jana  alipokuwa akikabidhi viti  75 na meza 75 vilivyotengenezwa na wazazi katika kukabiliana na matatizo ya  upungufu wa madawati ,meza pamoja na ukarabati wa madarasa mawili yaliyogharimu million  zaidi ya millioni 50

Alisema kuwa  wazazi wa vijiji vya kilimamoja, huduma na chemchem wamefanya hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utoaji wa elimu bure kuanzia  shule ya msingi na mpaka kidato cha nne kwa  sekondari.

Kayanda alisema faraja pekee wanayopata wazazi ni kuona vijana wao wanafaulu, na wanaendelea na elimu ya juu, nakusema wanafunzi wametengenezewa mazingira mazuri zaidi ya kusoma hivyo ni  lazima sasa walimu waongeze jitihada katika kuondoa daraja sifuri.

 Aliongeza kusema kama ufaulu utaongezeka hata shida ya ujenzi wa jengo la utawala inaweza kutatulika kwani wazazi watapata moyo wa kuendelea kujitoa kwa ajili ya watoto wao, ambapo aliomba walimu kuongeza ufuatiliaji wa wanafunzi kwa  kushirikiana na wazazi pindi wanapobaini matatizo ya mtoto katika maendeleo yake ya kitaaluma. 

Kayanda amepongeza uongozi wa serikali ya kijiji kwa  kusimamia maagizo ya serikali ya kukarabati na kumalizia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa,  ukarabati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa umezingatia vigezo na umetoa picha nzuri kwa  serikali na umesaidia kuondoa matatizo ya uhaba wa vyumba vya madarasa.

Aidha  ametumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo ili kupata matokea mazuri kwani taifa linauhitaji wa wataalamu mbalimbali na wataalamu wanajengwa kutoka shuleni, huku akiwataka wanafunzi kuweka mkazo mkubwa katika masomo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Karatu  Abbas Kayanda ametembelea shule msingi ya Africa Galleria na kukabdidhi madawati 65 yaliyojengwa muwekezaji wa Africa Gallleria ,Madawati hayo yamesaidia kupunguza tatizo la  uhaba wa madawati katika shule hiyo ya msingi ,huku  akimpongeza muwekezaji Africa Galleria kwa kukumbuka kurudisha kwa jamii, jambo ambalo linazidi kujenga mahusiano chanya na jamii.

Akiwa katika shule ya Msingi Kainam Rhotia Kayanda amekabidhi madawati 48 ambayo yamejengwa na kukarabatiwa na wazazi katika shule hiyo ,amepongeza  wazazi kwa kuwa na mutikio chanya na kuhamasishana katika shughuli za maendeleo lengo likiwa ni kusaidia taasisi zinazozunguka maeneo yao.

Sambamba na kutembelea miradi ya elimu pia ametembelea zahanati ya Kainam Rhotia ambayo imepewa kiasi cha million sita kwenye fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka, ukarabati wa maabara na ujenzi wa jengo la choo ambapo  ameelekeza uongozi wa halmashauri ya kijiji kuepuka matumizi mabaya ya ununuaji wa vifaa vya ujenzi. 

Alisema kumekuwa tabia ya watendaji kuweka gharama kubwa za Quotation za miradi, gharama ambazo haziendani na bei ya uhalisia ya ujenzi wa jengo, ambapo alitumia muda huo ameelekeza wataalamu kujiridhisha thamani ya bei za ununuaji wa vifaa vya ujenzi, ambapo pia aliutaka uongozi wa kijiji kusimamia na  kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme inaunganishwa katika zahanati hiyo mapema.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo diwani wa kata ya Rhotia Marsel Magasi alisema ziara ya mkuu wa wilaya imezidi kuwapa hamasa ya kusimamia shughuli za maendeleo, ili kata iwe na uwezo wa kufanya shughuli zake lazima kuwe na ushirikiano wa viongozi wakijiji katika kila eneo ambao watasaidia  kuibua na kutatua matatizo yatakazowasilishwa katika ngazi ya kata.M

Magasi ameshukuru wananchi wa kata ya Rhotia kwa kujitoa katika kutekeleza shughuli za maendeleo , Zahanati ya Kainam Rhotia itakapokamilika itasaidi kusogeza huduma za afya karibu zaidi ,ameuomba uongozi wa kijiji cha Kainam Rhotia kuweka nguvu katika ujenzi wa  zahanati ili uweze kukamilika kwa wakati.

Share To:

Post A Comment: