NA ANDREW CHALE


MDAU wa Maendeleo, Godfrey Maduhu kwa kutambua mchango wa Walimu hapa nchini ameamua kusaidia viti maalum vya kukalia Walimu shule ya Msingi Gezaulole iliyopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.


Maduhu ameeleza kuwa, Walimu wamekuwa na mchango mkubwa katika makuzi ya Watoto kitaaluma ambapo pia wamekuwa wakikabiriana na changamoto ya vifaa na vitendea kazi.


"Walimu wana mchango mkubwa sana. Tumeshuhudia wakikaa kwenye viti visivyo na ubora na hata wakati mwingine kukalia madawati ya wanafunzi.


Kwa kuliona hilo nikiwa kama mdau wa maendeleo nachangia viti 23 ili visaidie na kuwaongezea  ufanisi hapa shuleni." Alieleza Godfrey Maduhu.


Kwa upande wa Uongozi wa shule ukiongozwa na Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bi Mariam Kinande walishukuru kwa msaada huo huku wakiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia 


"Msaada wa viti hivi una thamani kubwa sana kwetu. Walimu tumefarijika sana kwani vitatusaidia kwa kutuwekea mazingira mazuri ya kufundishia.


Tutaendelea kujitoa zaidi na zaidi katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka" Alisema Mwalimu Mkuu  Bi. Mariam Kinande kwa niaba ya Walimu.


Shule ya Msingi Gezaulole ni miongoni mwa shule kongwe nchini ipo pembezoni mwa bahari ya Hindi katika mji wa Kale na Kihistoria wa Mbwa maji, Gezaulole. 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: