Juma Raibu Juma Ni diwani pekee amehudumu kwenye baraza la madiwani toka awamu iliyopita wakati ambao madiwani wote wakitoka upinzani na yeye pekee ndio alikua diwani anayetokana na Chama cha Mapinduzi,alikumbwa na misukosuko vitisho,Kuvunjwa Mguu na wapinzani,Kuvunjiwa vioo vya magari yake,Kutengenezewa kesi za feki za mauaji lakini kamwe hakutetereka alifanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa ,alipambana kuhakikisha anawatetea wana moshi na alipinga uovu wazi wazi bila kukata tamaa,sambamba na kwamba alikua peke yake hakukata tamaa Bali alizidi kusonga mbele kwa kuchapa kazi kwa bidii na muda wote wa uongozi wake amekua mtetezi wa wananchi wanyonge.Juma Raibu Ni miongoni mwa hazina ya viongozi vijana katika taifa,kwa kweli UVCCM tunalo jambo la Kujivunia kutoka kwake na kuwa na kijana Mwadilifu wa caliber yake,Ndugu zangu wa Kaskazini hasa moshi mjini tunawaonea wivu sana kwa Kuletewa jembe hili la Kazi.


Kipekee sana Nimpongeze Mwenyekiti wetu *Dkt John Pombe Magufuli* ile siku ya Kampeni zake ushirika aliuvunja Mpango haramu uliokuwa umetegwa dhidi ya Juma Raibu lakini Mwenyezi Mungu alimtumia Rais Kama Nabii wake ili kumwokoa mjoli wake Juma Raibu


Kipekee pia niwashukuru wajumbe wa Kamati Kuu kwa Maamuzi ya Kulileta jina pekee la Juma Raibu maana Bila Maamuzi hayo Inawezekana Ule mpango haramu ungeweza kumharibi juma Raibu na tukaikosa Huduma Yake Katika manispaa Ya Moshi.


Niwape pole nyingi wala Rushwa,wapinzani,Wapiga madili kuwa Manispaa ya Moshi sio pango la Walanguzi Tena watafute  pa kukimbilia


Hitimisho nivishukuru vyombo vya usalama vya Chama Na serikali kwa kung'amua mitego michafu iliyopangwa kumwangamiza Kijana huyu mdogo na kuitupilia mbali.


Kachape kazi Mwana UVCCM mwenzangu Juma Raibu natambua Uchungu ulionao kuhusu Moshi

Share To:

msumbanews

Post A Comment: