Mwekezaji wa ndani anayemiki bar ya vyakula na vinywaji inayojulikana kama The Picnic (Ngome Kongwe) iliyopo Kaloleni jijini Arusha Antony Urasa ameishauri jamii inayotoa huduma kama zake kuboresha huduma zao ili kwendana na wakati na kuvutia wageni mbalimbali wanaoingia mkoani hapa wakiwemo watalii.

Rai hiyo ameitoa  wakati akiongea na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa mwonekano mpya wa bar  hiyo maarufu jijini hapa,baada ya kuifanyia maboresho makubwa yaliyoibadili mwonekano na kuwa na hadhi ya kisasa.

Aliwashauri wawekezaji wengine kuiga mfano huo ili kujenga mazingira ya kuvutia wateja na kupendezesha jiji la Arusha ambalo lina pilikapilika nyingi za utalii.

"Tumeamua kuboresha huduma zetu na mwonekano wa bar yetu ili iwe ya kisasa kwendana na wakati kwani tangu imeanzishwa mwaka 1978 imekuwa ikifanyiwa ukarabati wa kawaida tofauti na haya maboresho ya sasa" Amesema Urasa.

Urasa amesema kuwa bar hiyo kwa sasa itakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 200 waliokaa huku huduma za nyama choma,vyakula mbalimbali vikiwepo vya asili vikipatikana pamoja na vinywaji vya aina mbalimbali .

Alisema kuwa kabla ya maboresho hayo bar hiyo ilikuwa na uwezo wa kupokea wateja wapatao 100 huku wengi wao wakisimama ila kwa sasa inauwezo wa kupokea wateja 200 waliokaa kwa mkupuo mmoja.

Naye meneja wa bar hiyo, Bodia Kaaya amesema kuwa kwa sasa bar hiyo itatoa huduma Massa 24 na imeweza kuajiri wafanyakazi wapatao 40 wenye ajira ya moja kwa moja huku wengine wakiwa kwenye mchakato wa kuajiriwa

Mmoja ya wateja wa bar hiyo ,Emmanuel Maziku amesema kinachomvutia kufika katika bar hiyo ni huduma nzuri zinazotolewa na wahudumu wa bar hiyo akidai kuwa ndizo zinazomvutia yeye na viongozi mbalimbali wa serikali wanaofika kwa ajili ya kupata huduma za vyakula na vinywaji .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: