Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Delphina Patrick Mngazija , akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni wakati akiomba kura kwa Wananchi wa Kata ya Kinyagigi juzi.  
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Delphina Patrick, akiserebuka na Wananchi baada ya kuhutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni Kata ya Kinyagigi juzi.  
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa hadhara wa kampeni Kata ya Kinyagigi.
 




Na Ismail Luhamba, Singida.


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Delphina Patrick  Mngazija amesema akipata ridhaa ya kuchaguliwa atahakikisha anaimarisha Sekta ya Afya, Elimu, Maji na Nishati katika jimbo hilo.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kinyagigi kwenye mwendelezo wa kampeni zake za kunadi sera za chama hicho, mgombea huyo  ametaja vipaumbele vinne ambavyo atavitekeleza akichaguliwa.

“Wananchi mnaonisikiliza hapa napenda kuwaambia kwamba nina mambo makubwa manne ya kuwafanyia katika kipindi cha miaka mitano endapo mtanipa ridhaa ya kuwaongoza nitaanza na Sekta ya Afya, Elimu, Mifugo na Maji.” alisema Patrick.

Delphina akizungumzia suala la Afya alisema atahakikisha kila Zahanati iliyojengwa na Serikali inakuwa na vifaa tofauti na sasa ambapo kuna majengo tu huku kukiwa hakuna vifaa tiba vya kutosha.

“Ifikapo Oktoba  28 siku ya  Jumatano mjitokeze kwa wingi kupiga kura ili kuhakikisha tunakiweka chama chetu cha CUF madarakani ili tuttimiize ahadi tulizo ziahidi.” alisema .

 Hata hivyo hakusita na kutokuwa mchoyo wa fadhira kwa mwanamke mwenzake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa kazi nzuri alizozifanya kwenye Sekta ya Afya katika Serikali ya Awamu ya tano, hivyo nichagueni  na mimi nitakua kama Ummy.

Pia Mwalimu Delphina alisema kama watapata ridhaa ya kuongoza katika Jimbo la Singida Kaskazini ndani ya miaka hiyo mitano watahakikisha wanasimamia vyema masuala yote yanayowahusu wafugaji na wakulima, kutunga na kutengeneza sera bora ili kuwa na ufugaji wenye tija na kilimo kwa ujumla.

“Hakika nawaambia wananchi wangu chagueni Chama cha Wananchi ((CUF) ili kiende kushirikiana na wataalamu wa kilimo, maafisa mifugo tufuge na tulime kisasa ili tuondokane na umaskini tulionao, sasa ifikapo Oktoba 28 msifanye makosa kwa mgombea urai wetu Prof. Ibrahim Lipumba,  mimi na diwani wetu.” alisema Patrick.

Akifunga mkutano huo,  Mwenyekiti wa chama hicho,  Wilaya ya Singida, Shabani Jumanne, aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za mgombea ubunge na anaamini wamemuelewa na Oktoba 28 watakwenda kufanya maamuzi ya haki kukipatia kura chama chicho.

"Nimefurahi sana tumefanya mkutano wetu kwa amani ila napenda kuwaambia tusifanye siasa za mazoea twendeni tukafanye mabadiliko tumetawaliwa kwa muda mrefu sana bila maendeleo yeyote, hebu tazameni hatuna umeme, maji safi na salama, barabara mbovu chagueni chama cha wananchi  CUF kikaisimamie Serikali na kuhakikisha maendeleo haya yanapatikana katika jimbo letu." alisema Jumanne.

Share To:

Post A Comment: