Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina. akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi wa bwana shamba Respicius Paul.
Maabara ua Udongo inayotembea ambayo inatumika inapima Afya ya Udongo.

 Na Mariam Mwayela, Simiyu
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi  LuhagaMpina amevutiwa na uwepo wa Maabara ya udongo inayotembea ili kusaidia wakulima kupima afya ya udongo.
Akizungumza baada ya kutembelea banda la SUA katika Maonesho ya NaneNane, viwanja vya Nyakabindi, jana Mpin alisema metembelea banda la Wizara ya Kilimo pamoja na TARI  na kukuta kilio kikubwa kilichopo ni Maabara yaUdongo.
“Maabara ya udongo inaonekana ni kama kitu cha anasa lakini kwa vyovyote vile tunahitaji kupima afya ya udongo ili tuweze kuongeza uzalishaji wetu katika mazao ya kilimo.” alisema Mpina.
Aidha aliongeza kuwa maabara inayotembea ina gharama ndogo sana lakini inaweza kuhudumia Tarafa ama Wilaya nzima.
“Uzuri nimeambatana na Naibu Waziri wa Kilimo hivyo tutaangalia ni jinsi gani kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na TAMISEMI ili Halmashauri zote walau wawe na hizi Maabara zinazotembea ambazo zitawezesha ardi zetu kupimwa wakati wote katika mashamba ya wakulima wote”, aliongeza Mpina.
Mpina alisema SUA ina mambo mengi mazuri ikiwemo Teknolojia ya kuhifadhi chanjo kwenye chombo kinachotengenezwa ambacho kinatumia gharama ndogo sana ukitofautisha na vifaa tulivyozoea na vingine kuhitaji matengenezo makubwa ama umeme ukizingatia sio kila eneo la wafugaji lina umeme.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema kuwa anaishukuru SUA kwa kukubali kutumia maabara zake ya Udongo, Maabara ya Afya ya mbegu na Maabara ya Bayoteknolojia kuwezesha Maabara za Kilimo kutambulika Kimataifa ili kuweza kutoa huduma za kimaabara kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo.
Pia aliiomba SUA ishirikiane na Wizara ya Kilimo, TARI pamoja na Halmashauri kuhakikisha Maabara hizo za udongo zinazotembea zinapatikana.
Hadi sasa SUA imeweza kutoa maabara ya udongo inayotembea katika Halmasahauri ya Mvomero na tayari kuna mpango wa kupeleka katika Wilaya ya Njombe Mji na Mbeya Mjini.


Share To:

Post A Comment: