ImageNa John Walter-Babati

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Manyara inamshikilia afisa uchumi wa Halmashauri ya mji wa Babati kwa tuhuma ya kugawa  maeneo ya kujenga vibanda katika uwanja wa Kwaraa , kiwanja kimoja  akipewa zaidi ya mtu mmoja hali inayosababisha sintofahamu miongoni mwa wananchi.
Mchumi huyo anaetajwa kwa jina la Colaman Urasa anadaiwa kugawa maeneo hayo  ambayo halmashauri ya mji wa Babati iliamua kuwapatia watu wenye uhitaji wa kujenga majengo kwa ajili ya biashara kulingana na mikataba waliyokubaliana.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu akithibitisha kushikiliwa kwa afisa huyo, amesema katika uchunguzi wao wamebaini kuwa Urasa ambaye amepewa jukumu la kusimamia upimaji na ugawaji amekuwa akigawa maeneo hayo kwa wananchi waliotimiza masharti kama yalivyoainishwa na halmashauri.
Amesema baadhi ya wananchi waliofika katika maeneo yao kwa lengo la kuanza  shughuli za ujenzi hukuta maeneo hayo yapo kwa watu wengine na kuanza ujenzi hali inayopelekea sintofahamu kati ya wananchi ambao huona kama halmashauri imewatapeli.
Makungu amesema kwa mujibu wa sheria Urasa ametenda kosa la matumizi mabaya ya  madaraka chini ya kifungu cha 96 cha Penel Code.
 Amesema bado wanaendelea na uchunguzi juu ya thuma hizo na mara utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.
Aidha Takukuru imewataka wananchi wengine waliokumbana na adha kama hiyo ya maeneo ao waliyopewa kutolewa kwa watu wengine wafike ofisi za Takukuru Babati Julai 13,2020 ili tuhuma dhidi ya Colman Urasa zishughulikiwe kwa ujumla wake.
Hata hivyo mkuu wa Takukuru ameeleza kuwa halmashauri ya mji wa Babati imepeleka wataalamu katika eneo hilo la Kwaraa, kusimamia upimaji na ugawaji  ili kudhibiti ujenzi holela.
Share To:

Post A Comment: