Benki
 ya Exim yatangaza likizo ya malipo ya mikopo yenye thamani ya Shilingi 
bilioni 160 kwa wateja wake ili kuwanusuru na athari za janga la COVID -
 19.
Benki
 ya Exim imetangaza msamaha wa likizo ya malipo ya mikopo kwa wateja 
wake wakubwa, wa kati na wadogo walipo katika sekta zilizo athirika 
zaidi kiuchumi kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa virus vya 
Corona (COVID 19). Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea 
kuchukuliwa na benki hiyo katika kuwasaidia kifedha wateja wake waliopo 
sekta ambazo zimeathiriwa zaidi na athari za mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa
 mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki 
ya Exim, Bw Jaffari Matundu alisema msamaha huo wenye thamani ya zaidi 
ya sh Bilioni 160 umeanza mwezi Juni mwaka huu, ukihusisha likizo ya 
malipo ya mikopo kwa wateja na nyongeza ya muda wa urejeshaji wa mikopo 
ili kusaidia wateja wa benki hiyo katika sekta mbali mbali kutokana na 
athari za janga hilo kwenye biashara zao.
"Benki
 inaelewa mahitaji ya wateja wetu wakati huu na tunafanya yote 
yanayowezekana kuwasaidia ili waweze kuvuka salama katika kipindi hiki 
kigumu. Jitihada hizi haziishii tu kwenye misamaha hii tunayoitoa bali 
pia kupitia huduma za ushauri kuhusu mikakati ya biashara ili 
kuhakikisha kwamba biashara za wateja wetu zinadumu na zinafanyika kwa 
mafanikio zaidi,'' alisema.
Kwa
 mujibu wa Bw Matundu msamaha huo unazingatia vigezo mbalimbali kwa kila
 mteja kwa kuwa athari za COVID-19 hazikuwa sawa katika sekta zote. 
"Tunafarijika kwa kuwa tayari wateja waliopo kwenye sekta zilizoathiriwa
 zaidi wameshaanza kusaidiwa. Mazungumzo na wateja wengine bado 
yanaendelea ili kutambua hatua mbali mbali zinazofaa kulingana na aina 
ya biashara, " aliongeza.
"Siku
 zote Benki ya Exim, tunaamini katika kufanya kazi kwa bidii leo kwa 
ajili ya kesho bora kwa wateja wetu, biashara zao na jamii kwa jumla, ni
 kwa mtazamo huo tumepitisha hatua kama hii katika wakati huu 
mgumu.Tunaendelea kujitolea kushughulikia mambo haya na kupata suluhisho
 sambamba na mamlaka pamoja na Serikali katika kuhakikisha uchumi wetu 
unaendelea kuwa thabiti wakati wa nyakati hizi ngumu. " alihitimisha.
Post A Comment: