Waandamanaji mjini Minneapolis nchini Marekani wamepambana na polisi wa kutuliza ghasia kwa usiku wa pili mfululizo kufuatia hasira ya umma inayotokana na kifo cha kikatili cha mmarekani mweusi aliyekuwa chini ya mikono ya polisi. 

Hasira ya umma inatokana na video iliyorekodiwa na mpita njia siku ya Jumatatu ikionesha polisi mzungu akitumia goti kumkandamiza shingoni mwanaume mmoja mweusi aliyefungwa pingu huku akiomba msaada kutokana na kukosa pumzi. 

Siku ya pili ya maandamano iliyoambatana na visa vya wizi na uharibifu wa mali ilianza saa chache tangu meya wa mji huo alipotoa wito kwa waendesha mashtaka kufungua kesi ya jinai dhidi ya polisi huyo aliyesababisha kifo cha George Floyd. 

Mauaji ya kiholela ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ambayo yanatekelezwa na polisi wazungu nchini Marekani yameongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni nchini humo.
Share To:

Post A Comment: